Tuesday, October 4, 2011

NANI NI MKWELI KATIKA HUU MKANGANYIKO?

Bi. Mwanahawa Ally

Rais wa Five Stars Modern Taarab "Ally Jay" (kushoto)
Takribani wiki mbili zilizopita Kumekuwa na maswali yasiyo na majibu katika vichwa vya watu hususan kwa wapenzi na mashabiki wa muziki wa Taarab hapa nchini, kuhusiana na Bendi ipi ambayo ina mkataba halali wa kufanya kazi na Mwanamuziki mkongwe wa Muziki huo wa Taarab hapa nchini Bi. Mwanahawa Ally.
Mkanganyiko huo umetokea mara baada ya tetesi kuwa Mwanamuziki huyo amejiunga rasmi na Kundi jipya la Tanzania motto modern Taarab na muda mfupi baadae kukaibuka tetesi kuwa mwanamama huyo amejiunga na kundi la Five Stars Modern Taarab na hatimaye wiki moja baadae mkurugenzi wa kundi hilo Mr. Yusuph pamoja na Rais wake Ally Jay kuweka bayana kwa waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari habari kuwa mwanamuziki huyo kwa sasa amehamia katika kundi lao la Five Stars Modern Taarab, lakini cha kushangaza wiki moja baadae akaibuka Mkurugenzi wa Tanzania Motto Modern Taarab na kueleza kuwa mwanamuziki huyo ni wa kwake na ana mkataba nae hivyo hatomruhusu kupanda kwenye Stage ya kundi lolote isipokuwa kundi la Melody Modern Taarab mpaka pale watakapolizindua rasmi kundi hilo Oktoba 30 mwaka huu.

Baada ya mkanganyiko huu ambao unachanganya vichwa vya watu Afrobeat imeamua kutafuta ukweli kwa kuwaunganisha Bi Mwanahawa Ally mwenyewe, Rais wa Five Stars Ally Jay pamoja na Mkurugenzi wa Tanzania Motto Amini Salmin ili waeleze ukweli uko wapi?????  sasa ili kufahamu ukweli wa jambo hili usikose kuangalia Afrobeat ya Eatv Jumamosi hii saa moja jioni.

No comments:

Post a Comment