Monday, October 3, 2011

MAADHIMISHO YA SIKU YA WAZEE DUNIANI MKOANI LINDI, YALINOGAJEEEE?

Wazee hawa wa katikati huwa wananifurahisha sana maana wako mbele katika kila shughuli iwe msiba, harusi na shughuli zingine za kijamii wa pili kushoto anaitwa bint Rajab na wa pili kutoka kulia anaitwa mama Nakanganigwe hao wengine wameficha sura zao sijawapata vizuri. Hapo katika mbio za kukimbia na magunia.

Wanaume nao hawakupitwa wakaingia mzigoni, kule nyuma kulia namuona mzee Terela na huyu wa mbele kushoto tulikuwa tunamuita mzee Kifimbo maana kila wakati alikuwa akitembea na fimbo na kututishia wakati tukiwa watoto, but jina lake halisi silifahamu na hapo nimewakumbuka wawili pia.

Sasa kazi ikahamia kwenye kuvuta kamba mwenye nguvu ndo anaonekana hapo na kama wala ugali wa bure pia twakugundua hapo.

Baada ya wanawake wanaume nao wakaingia kuonyesha nao wamezeeka nywele tu na si vinginevyo.
Picha: Na mdau Abdulaziz wa Lindi Press Club

No comments:

Post a Comment