Wednesday, October 12, 2011

BENKI YA NBC YATOA MSAADA WA VIFAA VYA MAABARA SHULE YA SEKONDARI ILULU MKOANI LINDI

Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzira akipokea msaada wa vifaa vya
maabara kwa ajili ya shule ya sekondari ya wasichana wa mkoa wa
Lindi(Ilulu sekondari) Vilivyotolewa na NBC.Kulia anayekabidhi msaada
huo kwa Niaba ya NBC,Rademptus Masanja wa NBC Makao Makuu, Makabidhiano
hayo yalifanyika katika Maabara ya shule hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Ludovick Mwananzira akikabidhi msaada uliotolewa
na NBC kwa Mkuu wa shule ya sekondari ya wasichana Ilulu, Mwl Sarah
Mlaponi

Masanja akifungua moja ya box la vifaa vya maabara vilivyokabidhiwa
ilulu sekondari na Benki ya NBC

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki akiishukuru benki ya
NBC kwa kutekeleza ombi lake la vifaa vya maabara kwa shule hiyo,Kulia
ni Mbunge wa Kilwa kaskazini,Murtaza Mangungu,Ludovick Mwananzira,Mkuu
wa mkoa wa Lindi na mwisho ni mwakilishi wa benki ya NBC,Bw Masanja

Mkuu wa Mkoa wa Lindi akisalimiana na wanafunzi wa shule ya Sekondari
ya wasichana wa Mkoa wa Lindi mara baada ya kutambulishwa katika ziara
ya makabidhiano ya Mkoa baada ya Rais JK kufanya mabadiliko na baada
ya wiki mbili toka aapishe wakuu wa mikoa huku wakiwa wameanza kazi
Amebadilisha kati ya Shinyanga na Lindi

No comments:

Post a Comment