Monday, October 17, 2011

Mkuu wa mkoa wa lindi, Bw. Ludovick Mwananzira akipata maelezo
kuhusiana na mafuta ya ufuta katika banda la chama kikuu cha ushirika
mkoa wa lindi(Ilulu) alipokuwa akikagua mabanda ya maonyesho ktk
kilele cha siku ya chakula duniani kitaifa mkoani lindi

Wakuu wa wilaya za mkoa wa lindi wakisikiliza hotuba ya
maadhimisho ya siku ya chakula mkoani humo, kutoka kulia,Bi Hawa
mchopa ,mkuu wa wilaya ya Ruangwa,Elias Goroi-Nachingwea na mwisho
mkuu wa wilaya ya Liwale, Paul Chiwile

Mkuu wa mkoa wa lindi akipata maelezo kutoka kwa
wajasiriamali wa manispaa ya lindi

Wadau wa habari nao wakiwa wanaokota baadhi ya
matukio jirani na wakuu wa idara za halmashauri (huyu wa kwanza kulia hapa anaitwa Mwanja Ibadi)

Afisa kilimo wa wilaya ya Lindi Bw. Matunda akikagua Mashine ya kusaga muhogo
Wakazi wa mji wa Lindi waliojitokeza siku hiyo wakishuhudia baadhi ya wasanii waliotumbuiza kwenye maadhimisho hayo

Wadau wakifuatilia matukio kwa umakini kabisa jamani wadau (wa kwanza kushoto hapo ni mama yangu mkubwa)

Maadhimisho ya siku ya chakula duniani kitaifa yamefanyika
mkoani LINDI jana kwa lengo la kutoa nafasi ya kutafakari jinsi jamii
katika ngazi zote zinavyoweza kuhakikisha uzalishaji na upatikanaji wa
chakula cha kutosha chenye lishe bora  kwa wakati wote na kwa bei
nzuri kwa wote.


Akihutubia katika Maadhimisho hayo jana, Kwa niaba ya Waziri wa kilimo na Chakula,Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Ludovick Mwananzira amewataka wakazi wa mkoa huo kuacha matumizi mabaya ya chakula kidogo kinachopatikana na badala yake kutumia kwa uangalifu ili kuondoa tatizo la njaa linaloweza kuukumba mkoa huo.


Sambamba na hilo Mwananzira alieleza jinsi Tanzania ilivyokumbwa na
mabadiliko ya bei za vyakula kunakochangiwa na bei za mafuta na
Nishati nyinginezo.

Naye Msaidizi Mwakilishi mkazi wa shirika la chakula na kilimo la
Umoja wa Mataifa(FAO), Bw Gerald Runyoro akitoa taarifa ya Umoja huo
alielezea sababu zinazosababisha kuwepo kwa watuwenye njaa zaidi ya Bilioni moja
Duniani.

Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa mkoa huo Licha ya kuishukuru Wizara
kwa kupanga maadhimisho hayo Mkoani Lindi hawakusita kueleza masikitiko yao kwa kutokuwepo kwa hamasa juu ya Maadhimisho hayo yaliyokuwa na wawakilishi na wakazi wachache waliohudhuria.


Maadhimisho hayo pia yaliambatana na maonyesho ya vitu mbalimbali vya
chakula huku Kauli mbiu ya Maadhimisho ya siku ya chakula duniani kwa
mwaka huu,  ikisema "Bei za vyakula kutoka kuyumba hadi kutengemaa".


Habari hii imeletwa na: Mdau Abdulaziz Video kutoka Lindi

No comments:

Post a Comment