Friday, March 23, 2012

DADA AZIMIA BAADA YA KUTAPELIWA SHILINGI 75,000

Dada mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana alipoteza fahamu baada ya kugundua kuwa ametapeliwa pesa kiasi cha shilingi elfu 75 pamoja na simu yake ya mkononi na watu wasiojulikana(Pichani ni akina mama wakisaidia kumnyanyua dada huyo ili kumuweka sehemu salama)

Tukio hilo lilitokea maeneo ya Quality Centre ambapo dada huyo alikwenda kwa matembezi yake ndipo akakutana na vijana wawili ambao walijitambulisha kwake kuwa wanauza madini, dada wa watu akatamani wakaanza kubargain wakafikia bei waliyokubaliana dada akatoa pesa kiasi cha Tshs 75,000 na simu yake ya mkononi ambayo hakusema ni ya thamani gani.
Baada ya wale jamaa kuondoka ndipo akagundua kuwa hayakuwa madini bali ni mawe madogo madogo manne(Pichani ni moja kati ya hayo mawe akiwaonyesha watu waliokuwa kwenye tukio)
Haya nayo ni kati ya hayo mawe manne
Baada ya kugundua kuwa ametapeliwa ndipo akapoteza fahamu, akifikiria simu yake na pesa zake zimepotea bure(Pichani ni huyo dada akisimulia tukio zima lilivyokuwa mpaka yeye kupoteza fahamu)
Baada ya kusimulia mkasa mzima na kupata nguvu dada wa watu huyooo akaondoka.. Huu wizi upo siku nyingi sana na sidhani kama kuna mtu afahamu kuhusiana na hili, sijui tatizo ni tamaa au wengine wageni mjini mimi na wewe hatujui ila la msingi tunatakiwa kuwa makini sana na hili jiji maana kila mmoja ana namna yake ya kutafuta riziki ndo maana wanasema mjini shule........ Ahsanteni wadau Andrew na Angel wa FNB Quality Center kwa picha na habari hii            


No comments:

Post a Comment