Monday, March 12, 2012

MAKAMBA AZUNGUMZA NA SUPER MIX LEO

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini Tanzania, Mh. January Makamba amesema kamati yake imejipanga kuhakikisha kuwa taifa haliingi gizani tena kama ilivyokuwa hapo nyuma.


Akiongea leo kwenye kipindi cha Supa Mix cha East Africa Radio Mh. Makamba amesema kamati yake inayoendeshwa na yeye ambae ni kijana kamwe haitorubuniwa na kuingia katika mitego ya kununuliwa na makampuni ya kigeni.


Mheshimiwa Makamba pia amezungumzia suala la kuwezesha vijana kupata elimu ya nishati ya mafuta na gesi ambapo kamati yake imetoa maelekezo kwa TPDC kutumia fedha za mafunzo zipatazo dola milioni 1.8 zinazotolewa kila mwaka na makampuni ya mafuta vijana

No comments:

Post a Comment