Thursday, March 22, 2012

WATANZANIA TUWAUNGE MKONO CHANETA

Leo ofisini kwetu tumepata wageni ambao ni Mke wa Waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania mama Tunu Pinda na mke wa Mheshimiwa Waziri Lukuvi wakiongozana na mwenyekiti wa Chama cha Netball Tanzania (Chaneta) Mama Filbert Bayi lakini lengo kuu ni kuitikia mwaliko wa kipindi cha Wanawake Live kinachoongozwa na Joyce Kiria.. Mengi kati ya mambo ambayo wamezungumzia ni pamoja na mikakati iliyopo katika kuiwezesha timu ya Taifa ya Netball iweze kufanikiwa na kupata ushindi katika mashindano ya Netball ya Nchi za Afrika ambayo yanatarajiwa kufanyika May mwaka huu ambapo Tanzania ndiyo wenyeji wa Mashindano hayo.

Wanasema ukikaa karibu na waridi basi nawe utanukia, na siye tukasema tujisogeze karibu kutoka kushoto ni mimi(Kijah), mama Lukuvi, Mama Bayi, Prudence wa 5Connect, Mama Pinda na Joyce Kiria
Watu kama hawa wakipatikana basi kila mtu anajitahidi kufanya la kwake maana si unajua majukumu mengi hivyo upatikanaji wao ni wa nadra sana ITV nao wakasubiri weee baada ya kumaliza wanawake Live tu wakawadaka, hapo pichani ni Mama Bayi ambae ndo mwenyekiti wa Chaneta akifanya mahojiano na ITV kuhusiana na wapi walipofikia katika maandalizi ya mashindano hayo ya May.

No comments:

Post a Comment