Thursday, March 22, 2012

MILLEN MAGESE KUSAKA WANAMITINDO

Mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania, Millen Happiness Magese ataendesha zoezi la kutafuta wanamitindo wawili (kwa vijana wa kike na kiume) watakoshiriki kwa mara ya kwanza katika maonyesho ya wiki ya Mavazi ya Afrika Kusini (South Africa Fashion Week) tarehe 1 April mwaka huu.
Millen atafanya zoezi hilo kupitia kampuni yake ijulikanayo kwa jina la Millen Magese Group Company Limited chini ya mpango wake wa kuitangaza Tanzania kupitia fani ya mitindo (Tanzania International Fashion Exposé (TIFEX).
Alisema kuwa wanamitindo wanaotaka kupata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika SAFW kufika siku ya Jumapili tarehe 25 mwezi huu kwa ajili ya mchujo huo kuanzia saa 8.00 mchana kwenye hotel ya Serena.

Alifafanua kuwa anaamini kuwa wanamitindo wa Tanzania watakaopatikana katika zoezi hilo wataiwakilisha Tanzania vyema katika wiki ya maonyesho ya mavazi ya Afrika Kusini na kuitangaza Tanzania kimataifa kama anavyofanya yeye kwa hivi sasa. 
Alisema kuwa hiyo ni fursa pekee kwa wanamitindo kuweza kujitangaza wenyewe kimataifa na kufuata nyayo zake.
 Zaidi bofya hapa

No comments:

Post a Comment