Thursday, March 8, 2012

UTAMBULISHO WA LILYAN INTERNET NA ALLY AKIDA ULINOGAJEEE

Jana jumatanomashujaa Musica waliandaa show maalum kwa ajili kuwatambulisha rasmi wanamuziki wao wapya ambao ni Lilyan Internet na Ally Akida, hivyo Afrobeat Team ilitinga pande hizo kwa ajili ya kupata matukio kwa ajili ya kuwajuza watazamaji wa kipindi na Blog hii pia(Hapo pichani ni Cameraman Rashid akirekebisha mambo kabla ya kurecord)



Show ilifanyika Nyumbani Lounge, hapo ndo nikiingia mdada
Baada ya kufika nikajoin na wadau wengine wakati tukisubiri Show ianze
Charles baba mwenye kofia naona yuko Busy mwenyewe cjui mambo ya BBM au anawaambia washikaji waje kuangalia Show.. Lol!
Meneja wa Mashujaa Musica Max anayekata maji na msaidizi wake Khamis
Kama kawaida show ikaanza kama unavyoona picha yenyewe inajieleza
Jado FFU Rais mstaafu
Kikazi zaidi
Big Boss Isaack Gamba na Salma Dakota kutoka Radio One Stereooo, hapo Lady Hanifa sijui alikuwa wapi
Wakinogesha mambo, maana bila hawa jamaa kusingekuwa na muziki ingawa hawavumi kama waimbaji wanavyovuma.
Malkia mwenyewe Lilyan Internet akapanda Stejini, hapo ndo wakati ameitwa kutoka huko alikokuwa amefichwa, baada ya kufika ndo akatengeneza Pozi hilo
Kazi imeanza, alikataje maunooo si unajua mambo ya Lily mwenyewe!! kama hujui tembelea Mashujaa Musica kila Ijumaa na Jumapili wanakuwa pale Business Park Victoria na Jumatano ndani ya Nyumbani Lounge
Ikafika zamu ya Ally Akida nae pia akatambulishwa (pichani ni Charles Baba akimtambulisha Ally Akida, mwenye Gitaa)
Baada ya kutoka Nyumbani Lounge, safari ikaelekea Club Sunciro hapo kulikuwa Listening Party ya Mashauzi Classic ambapo walialika baadhi ya wadau ili wasikilize Album yao na kuwashauri nini kifanyike kama kuna mapungufu yoyote kwenye nyimbo zao na Album yao hiyo ya kwanza inatarajiwa kuzinduliwa April mwaka huu.
Thabit Abdul na mpiga Gita mwenzake wakiwajibika
Mzuka ukawapanda sasa, yaani ilinogajeee walinifurahisha sanaaa
Mamaa Isha mwenyewe Rais wa wanawake wote wanaoweza kujitafutia, usishangae hiyo ni a.k.a yake mpya ya sasa.. Hapo akichonga na Afrobeat na kikubwa zaidi amewaomba mashabiki wanunue Album yao Original na siyo Feki ili waweze kuwainua kimuziki na wao watengeneze kazi nzuri zaidi.

Afrokija Blog inakutakia kila la kheri mama, mwenyezimungu akujaalie hiyo Album itoke na mashabiki wakuunge mkono kwa kununua kazi yako Original kama ulivyowaomba..... Nimemalizaaaaaaaa

No comments:

Post a Comment