Monday, March 5, 2012

LILYAN INTERNET NA ALLY AKIDA KUTAMBULISHWA JUMATANO HII

Ally Akida(kulia) na Abou Semhando kushoto

Lilyan Internet
 
Baada ya kusaini mkataba na Bendi ya Mashujaa Musica mwishoni mwa wiki iliyopita, waliokuwa wanamuziki wa Bendi ya African Stars(Twanga pepeta) mnenguaji Lilyan Tungaraza(Internet) na Mkung'uta gitaa Ally Akida wanatarajia kufanyiwa utambulisho maalum kwa wapenzi na mashabiki wa Bendi hiyo.
 
Akizungungumza na blog hii Meneja wa Mashujaa Musica Maxmillian Luhanga amesema, wanamuziki hao watatambulishwa rasmi Jumatano hii katika ukumbi wa Nyumbani Lounge.

Amesema utambulisho huo utasindikizwa na Bendi ya Machozi inayomilikiwa na mwanamuziki Lady Jaydee ambao ndiyo wenyeji wa Nyumbani Lounge. 
 
Aidha Luhanga amesema Bendi hiyo inayozidi kuwashika mashabiki siku hadi siku  hapa nchini imeshakamilisha albam yake ya pili na inayotarajia kuzinduliwa mapema may mwaka huu.
Luhanga ameongeza kuwa albam hiyo yenye nyimbo nane inakwenda kwa jina la TIKISIKA na nyimbo hizo ni pamoja na Umeninyima, ambao wameimba na Nguli wa Musiki wa dansi Papa Wemba.
Nyimbo nyingine ni Ungenieleza, kwa Mkweo, Penzi la Mvutano, Uchungu wa Moyo, Tikisika, hukumu ya Mnafiki wimbo ambao unawania tuzo ya Kili Muzic Award 2012 na wimbo wa mwisho katika albam hiyo ni Nipe Joto.

No comments:

Post a Comment