Tuesday, March 27, 2012

MBUNGE WA JIMBO LA MTWARA MJINI MHESHIMIWA HASNEIN MURJI AWAPIGA TAFU WANAMICHEZO WA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA -MTWARA

Mbunge wa Jimbo la Mtwara mjini (CCM) Mheshimiwa Hasnein Murji amekabidhi vifaa vya michezo na pesa Taslimu Tshs Milioni moja kwa Timu za michezo mbalimbali za Chuo cha Utumishi wa umma mkoani Mtwara kwa lengo la kuzisaidia timu hizo ziweze kufanya vizuri katika mashindano
ya  michezo ya  Vyuo vya Utumishi wa Umma nchini yanayotarajia
kufanyika mwanzoni mwa wiki ijayo Mkoani Tanga ambapo pia ameahidi kutoa kiasi cha Shilingi milioni moja kwa kila mchezo utakaopata ushindi katika mashindano hayo (Pichani :Vifaa vya michezo vilivyotolewa na Mh. Murji)

Mrs Moza Nassor,  Naibu waziri-Serikali ya chuo,Nahodha timu ya Netball

Kufuatia msaada huo,Rais wa Serikali ya wanachuo wa Utumishi
Mtwara,DAISY JAFARI(pichani)  pamoja na NAHODHA  wa Timu ya Netball ambae pia ni
Naibu waziri wa Michezo Chuoni,Bi Moza Nassor kwa pamoja wakiongea na
mdau wa blog hii Abdulaziz Ahmed waliwahakikishia wanachuo pamoja na Wana Mtwara kuwa
timu zao zitarudi na Ushindi kutokana na Ushirikiano walioupata katika
maandalizi ya michezo hiyo itakayoanza April 3 na kumalizika April 6 mwaka huu huko jijini Tanga na kushirikisha wanamichezo 50 kutoka kila tawi la Chuo cha Utumishi wa umma nchini kwa michezo ya mpira wa miguu, mpira wa pete, Volleyball na mpira wa kikapu
Mh. Murji (kulia) akikabidhi pesa taslimu Tshs milion moja kwa Kaimu
mkuu wa chuo, Bw SEME PETER
Mh. Murji akitoa nasaha zake kwa wanachuo
Mh. Murji akionyesha baadhi ya vifaa vya michezo alivyokuja navyo
Mh. Murji akionyesha pesa alizotoa katika kusaidia Timu hizo
Pesa zikikabidhiwa kwa wanachuo wenyewe

No comments:

Post a Comment