Friday, June 10, 2011

JAMANI WADAU HII NDIYO SIRI YA UREMBO NA KUPENDEZA KWANGU

Kuna watu wengi sana wakiwemo wadau na wapenzi wa Kipindi changu cha Afrobeat, ninaowasiliana nao aidha kwa email, simu na hata baadhi ya wale ambao nakutana nao katika mishe zangu za hapa na pale hususani niwapo LOCATION nikiwa nafanya maandalizi ya kipindi, wamekuwa wakiniuliza napata wapi nguo na Accesories ambazo huwa natupia kwa kuwa wanavutiwa nazo, sasa nikaona hao ni wachache tu ambao wameweza kupata nafasi ya kuuliza nikahisi wapo ambao hawajapata nafasi lakini nao wanavutiwa na wangependa kufahamu pia....... 

Jamani siri ya kupendeza kwangu na hata wewe ukipenda pia pita pale AMINA'S DESIGN pande za Kariakoo mtaa wa PEMBA/KONGO...


Hapa nakuonjesha tu baadhi ya maujanja yaliyopo.........
Mambo ya Accesories ndo hayo ya kila aina ushindwe wewe tu..
Kitu cha Clutch hicho viko vingi vya kila ainana kila rangi ila km nilivyosema na nawapa hamu kidogo mengi zaidi utayapata baadae kidogo
Coctail Ring za kumwaga na za kila aina kazi kwako tu waipenda ipi???
Hand bags pia ukipenda tena mambo ya mnyama km unavyojua kwa sasa ndo imerudi kwenye chati
Jamani vumbi na jua la bongo kali yafaa pia uyahifadhi macho yako kwa kitu miwani
Siku hizi wiggs si kwa waliokosa nywele tu hata wenye nywele hadi mgongoni nao aah wamo
Kwa madada do ndo hivyo tena km mnavyoona jamani
Msiopenda kubanwa pia msipate kisingizio mtahudumiwa pia
Niseme nini sasa na mambo ndo km haya kamili kila idara..... Usikose kupita km nawe wapenda kupendeza na uingie kwenye kundi la wadada na wamama wa mjini wanaojua kupendeza maana wote wapendezeshwa hapo, na utaingia kwa furaha na kuondoka kwa furaha zaidi sababu utahudumiwa kwa unyenyekevu, heshima na busara maana MTEJA kwao ni MFALME ndivyo wanavyosema...   PICHA kwa hisani ya WOMEN LIFE STYLE TREND


No comments:

Post a Comment