Friday, June 10, 2011

BAADA YA KUREJEA NYUMBANI KWA FURAHA, BHOKE AFUNGUKA KUHUSU UHUSIANO WAKE NA BOYFRIEND WAKE WA BONGO

Baada ya kutua ktk uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl J.K.Nyerere jijini DSM juzi jumatano ndugu, jamaa na marafiki  mbalimbali walijitokeza kumpokea ikiwemo Eatv Team na mama mzazi wa Bhoke.  Pichani juu ni  Zamzam wa Eatv ambae pia ni Best Friend wa Bhoke akimlaki  Bhoke mara baada ya kuwasili.
Akiwa na mama(Mzaa chema)
Baada ya kuwasili vyombo mbalimbali vya habari vilikuwa na hamu ya kufanya mahojiano na mwanadada, hapo pichani akihojiwa na Enewz ya Eatv.. Kikubwa ambacho alizungumzia hapo ni kuhusu kurudi kwenye kipindi chake cha 5Connect na maisha yake ya BBA kwa ujumla.
Kwa furaha kabisa akipozi na Jose Munthali a.k.a DVJ Joke moja kati Editors wakali wa Eatv a.k.a Prakata................ malizia mwenyewe
Akiiwakilisha vizuri Multichoice,anaitwa Barbara Afisa uhusiano wa Multi Choice
Baada ya Mahojiano na Eatv Bhoke aliendelea na mahojiano na vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini,ambapo katika moja ya mamboaliyoulizwa  ni kuhusu uhusiano wake na Boyfriend wake wa hapa bongo kabla ya kwenda BBA ambapo alijibu kuwa "hilo ni suala lake binafsi na ni yeye pekee ndiye ataweza kulisolve hivyo haoni umuhimu wa kulizungumzia zaidi"  na mipango yake ya baadae na Ernest na  kusambazwa kwa picha zao za BBA wakiwa Faragha alisema"Hawezi kuzungumza nini kitatokea baadae ila anachoweza kusema ni kwamba anapenda kuwa karibu na Ernest kama rafiki yake na kuhusu picha yeye hajali kwa sababu hawezi kuwazuia watu kusema ila kikubwa ameenjoy maisha Big Brother House. 
Crew nzima ya Eatv$EAR wakiongozwa na Radio Cordinator Nasser Kingu(kulia) wakiwa na Barbara na mama mzaa chema.




     

1 comment: