(PICHANI juu na chini ni Baadhi ya wanamuziki wa Msondo ngoma wakionyesha vitu vyao jukwaani)
Bendi kongwe ya muziki wa Dansi nchini, (MSONDO NGOMA) Baba ya muziki,IJUMAA hii inatarajia kufanya onyesho maalum lijulikanalo kwa jina la MTANZANIA JIVUNIE katika kijiji cha Makumbusho JIJINI DAR ES SALAAM.
Meneja wa Bendi hiyo SAID KIBIRITI amesema onyesho hilo maalum limeandaliwa na bendi yake kwa kushirikiana na uongozi wa kijiji cha MAKUMBUSHO, na Baada ya hapo bendi hiyo itakuwa ikipiga Show katika kijiji hicho kila siku ya IJUMAA
MAALIM GURUMO(Kiongozi wa Bendi)
Bendi ya Msondo ngoma kwa sasa inatamba na kibao kipya kijulikanacho kama SULUHU kilichotungwa na SHABAN DEDE, Hivyo idadi ya nyimbo mpya za msondo kufikia TANO ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya ALBUM yao mpya
SAID MABERA(Mpiga gitaa la Solo wa MSONDO)
KIBIRITI amewaomba wapenzi wa Bendi hiyo kujitokeza kwa wingi ili kuipa SUPPORT Bendi yao hiyo
ROMARIO kazini
Thursday, June 30, 2011
Wednesday, June 29, 2011
JAMANI TUTOE SUPPORT KWA NGOMA ZETU ZA ASILI
(Hapo juu na chini ni kikundi cha Jivunie kikitoa burudani ) |
Kuna tabia za baadhi ya watu kuona kuwa ngoma za asili ni kitu cha ajabu sana na wale wanaopenda kuhudhuria maonyesho ya ngoma hizo ni washamba au watu waliopitwa na wakati.
Tuesday, June 28, 2011
MAPACHA WATATU NDANI YA STEJI MOJA NA WAKALI WA BONGO FLEVA
ALLY KIBA |
BARNABA | Msanii mwingine ni ELIAS BARNABAS a.k.a BARNABA kutoka THT aliyetamba na vibao vingi km Mbalamwezi, SMS vingine vingi |
WAKONGWE WA MUZIKI TANZANIA KUTOA ALBUM YA NYIMBO ZA ZAMANI
(Abdul Salvador a.k.a Father Kidevu) |
Father kidevu na Kanku Kelly wa KILIMANJARO CONNECTION |
Wazee wakiwa mazoezini |
Babu njanje mazoezi yakiendelea |
Mzee Gurumo wa MSONDO NGOMA |
King Kikii na Ndalla Kasheba |
Baadhi ya Wakongwe wa Muziki TZ katika picha ya pamoja |
VIMWANA MANYWELE 2011 WATAMBIANA
Monday, June 27, 2011
AKUDO IMPACT KUTAMBULISHA NYIMBO ZAO MPYA
Bendi ya muziki wa Dansi, Akudo Impact a.k.a Vijana wa masauti wanatarajia kutambulisha nyimbo zao mpya zipatazo tano hivi karibuni |
NDOTO YA JAYDEE NA MTUKUDZI YATIMIA
Mwanadada anaetisha katika Game ya muziki BONGO ambae pia ni mmiliki wa Machozi Band, LADY JAYDEE amekamilisha ndoto yake baada ya kufanya ngoma na Mwanamuziki mkongwe kutoka Zimbabwe OLIVER MTUKUDZI, Ngoma hiyo ambayo ipo jikoni inafahamika kwa jina la MIMI NI MIMI imerekodiwa usiku wa Jumatatu iliyopita.
Lady Jydee na Oliver Mtukudzi kazini
Mazoezi inafaa pia siku moja nawe uweze kulichezea
Mazoezi muhimu kabla ya kuanza kazi
Mzungu kichaa nae alikuwepo
Siku za hivi karibuni JAYDEE NA MTUKUDZI waliwahi kufunguka kupitia Ting'a namba wani kwa Vijana EATV katika kipindi cha Afrobeat kila mmoja akidai kuwa ana ndoto ya kupiga kolabo na mwenzake
PICHA kwa Hisani ya Ladyjaydee.Blogspot
Lady Jydee na Oliver Mtukudzi kazini
Mazoezi inafaa pia siku moja nawe uweze kulichezea
Mazoezi muhimu kabla ya kuanza kazi
Mzungu kichaa nae alikuwepo
Siku za hivi karibuni JAYDEE NA MTUKUDZI waliwahi kufunguka kupitia Ting'a namba wani kwa Vijana EATV katika kipindi cha Afrobeat kila mmoja akidai kuwa ana ndoto ya kupiga kolabo na mwenzake
PICHA kwa Hisani ya Ladyjaydee.Blogspot
NAPE APOKELEWA KWA FURAHA MKOANI LINDI
Wajumbe wa mashina wa KATA zote 18 za wilaya ya Lindi wakifuatilia kwa umakini mkubwa KIKAO hicho |
NAPE NNAUYE akijumuika kutoa burudani na kikundi cha sanaa ya ngoma alipofanya mkutano wa Hadhara katika uwanja wa Fissi mjini Lindi |
Nape akiwapungia mkono kwa ishara ya kuwaaga wanachama wa CCM waliohudhuria mkutano |
NAPE akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi Bw. Ally Mtopa wakati wa mkutano wake wilayani Kilwa
PICHA KWA HISANI YA LINDI PRESS CLUB(LPC)
Thursday, June 23, 2011
M-NET YAZINDUA AFRICA MAGIC SWAHILI
M-NET AFRICA wameanzisha kituo kipya cha kurushia matangazo ambacho kimezinduliwa jana kinachofahamika kwa jina la AFRICA MAGIC SWAHILI.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa M-NET Biora Alabi, kituo hicho kitakachoanza rasmi Julai mosi kitakuwa kikirusha matangazo yake kwa Lugha ya kiswahili ili kuikuza Lugha hiyo, lakini pia itaonyesha Filamu na muziki wa Kiswahili tu.
Wawakilishi wa M-NET katika kukamilisha uzinduzi huo
Waalikwa waliohudhuria hafla hiyo ambayo imefanyika katika hotel ya MOVENPICK
Upande wa Tasnia ya Filamu nao hawakubaki nyuma walikuwepo kuwakilisha, hapo juu ni JB moja kati ya waigizaji ambao wananifurahisha sana
Aunt Ezekiel nae kama kawaida yake hapendi kuhadithiwa lazima ajionee mwenyewe.
Kanumba The Great mmoja kati ya waigizaji bongo nae alikuwepo, hapo akifafanua jambo
The Greatest nae akiwakilisha akiwa na Cloud
Mama lao katika movie Suzan Lewis nae akiwaongoza wanae
Mtu maarufu kwa kuiga sauti za watu Steve Nyerere nae akitema cheche zake
KWA WALE WAPENDA MOVIE ZA KIBONGO KAMA MIMI KAZI NI KWENU JAMANI KUIFUATILIA TU AFRICA MAGIC SWAHILI
Saturday, June 18, 2011
HALI YA BAMBO BADO NI TETE
Muigizaji na mchekeshaji mkongwe bongo ambae kwa sasa ni muajiriwa wa EATV kupitia ZE COMEDY SHOW, Dickson Makwaiyo a.k.a Bambo, ambae wiki iliyopita aliripotiwa kupata ajali ya pikipiki na kusababisha kuvunjika kwa mfupa sehemu ya goti hali yake bado si nzuri.
Pichani juu ni pikipiki na gari iliyosababisha ajali ya Bambo
Hali ya Bambo ilikuwa inaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji lakini katika hali isiyo ya kawaida habari zilizotufikia leo zinasema kuwa Bambo alianza kutokwa damu masikioni na baadae kufanyiwa uchunguzi zaidi na majibu zaidi yatapatikana kesho
Mtanga na Kicheko kutoka ZE COMEDY ya EATV wakimjulia hali Bambo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini DSM.
Pichani juu ni pikipiki na gari iliyosababisha ajali ya Bambo
Hali ya Bambo ilikuwa inaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji lakini katika hali isiyo ya kawaida habari zilizotufikia leo zinasema kuwa Bambo alianza kutokwa damu masikioni na baadae kufanyiwa uchunguzi zaidi na majibu zaidi yatapatikana kesho
Mtanga na Kicheko kutoka ZE COMEDY ya EATV wakimjulia hali Bambo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini DSM.
Subscribe to:
Posts (Atom)