Monday, June 3, 2013

MWILI WA ALBERT MANGWEA KUWASILI KESHO

Mwili wa marehemu Albert Mangwea utawasili kesho saa nane mchana ukitokea Nchini Afrika ya Kusini.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye kamati ya mazishi ya marehemu Albert Mangwea, kupitia msemaji wake Adam Juma, zinasema kuwa taratibu zote za kusafirisha mwili huo zimekamilika ambapo watanzania waishio nchini Afrika kusini nao wamepata nafasi ya kuuaga mwili wa marehemu hii leo na mwili huo utasafirishwa kesho ambapo utawasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu J.K Nyerere majira ya saa 8 mchana.

No comments:

Post a Comment