Friday, June 7, 2013

MUME WA KHADIJA KOPA KUZIKWA LEO NYUMBANI KWAO BAGAMOYO

Mama Mzazi wa mume wa Khadija Kopa Marehemu Jaffari Ally, Bi. Rehema Tuwa, akilia kwa uchungu kufuatia kifo cha mwanae.
Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki waliojitokeza kumfariji mama wa Jaffari nyumbani kwake Tandale
Baadhi ya viongozi na wananchi wa mkoa wa Rukwa na Mpanda wakimsindikiza kupanda ndege malkia wa mipasho Khadija Omar kopa kwenye uwanja wa ndege wa mpanda baada ya kupokea taarifa ya kifo cha mumewe, aliyefariki Dunia jana alfajiri Bi Khadija Kopa kutokana na maradhi, Khadija alikuwa akitokea kwenye Maadhimnisho ya siku ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa yaliadhimishwa Namanyere Mkoani Rukwa juzi. 
Mkuu wa mkoa Rukwa Eng. Stella Manyanya kushoto akimfariji Bi. Khadija Kopa alipokuwa kwenye chumba maalum cha wageni kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda.
Malkia wa Mipasho Khadija Omar Kopa akiwa na mumewe siku ya harusi yao.
Mume wa mwanamuziki wa Taarab na malkia wa mipasho Afrika mashariki Bi Khadija Omar Kopa, Jaffari Ally amefariki dunia majira ya saa 7 usiku wa kuamkia June 6 katika Hospitali ya Lugalo jijini Dar Es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa ndugu wa marehemu ni kwamba marehemu Jaffari amefariki baada ya kuugua ugonjwa wa kifua na kukosa pumzi siku kadhaa zilizopita lakini siku ya Ijumaa (May 31) hali ilizidi kuwa mbaya ambapo 
siku ya Jumatatu June 3 walilazimika kumkimbiza katika Hospitali ya Lugalo.

Ndugu huyo ameongeza kuwa alifanyiwa vipimo kati Hospitali hiyo lakini na cha kushangaza vipimo hivyo vilionyesha kuwa hakuwa na tatizo lolote, hivyo walilazimika kuchukua vipimo vingine katika hospitali ya TMJ ambavyo mpaka anafikwa na umauti bado majibu yalikuwa hayajatoka.


Hata hivyo taarifa zaidi zinasema kuwa mke wa marehemu, Bi Khadija Kopa ameruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Mwananyamala alikokuwa amelazwa kutokana na tatizo la Presha ya kushuka tangu alipoingia Dar Es Salaam kutokea Sumbawanga na tayari yuko Bagamoyo kwa ajili ya maandalizi ya mazishi ya mumewe yatakayofanyika leo saa 9 alasiri huko huko Bagamoyo.

Mwenyezi mungu ampe nguvu Bi Khadija katika kipindi hiki kigumu na ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, Amina

No comments:

Post a Comment