Uongozi wa Simba kuamua kumtema mchezaji wao Juma Kaseja
wamesema imetokana na maneno ya watu yanayoendelea huko mitaani, hali
inayosababisha wao kuamua kumuacha Juma Kaseja aende akajaribu sehemu nyingine.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, mwenyekiti wa Simba kamati ya usajili ,
Zakaria Hanspope alikuwa na haya ya kusema
“Unajua Juma Kaseja amechezea timu
ya Simba kwa miaka mingi sana, laikini hivi karibuni kumezuka maneno ya ajabu
kuhusu Juma Kaseja kuuza mechi anapokuwa uwanjani, kwahiyo kama uongozi tumeoa
hali hii haitoleta picha nzuri kwa timu yetu.
Kiongozi huyo alidai kuwa sababu
zingine hawatopenda kuziweka wazi ila kubwa ni kuhusiana Juma Kaseja
kutoaminiwa na baadhi ya mashabiki na kudai kuwa , kwa sasa anapocheza uwanjani
na timu zingine basi huwa anaamua kuuza mechi na kufungwa ili wapinzani waweze
kushinda.
“Kwahiyo kama viongozi wa simba
tumeona hali hii ya mashabiki kumsema kuwa Juma Kaseja anauza mechi kwa
wapinzani, itapunguza kiwango chake cha uchezaji, hata yeye anaposikia haya
maneno ile munkari ya kucheza inaisha kabisa sababu watu ambao anacheza
kwaajili yao hawamuamini tena” Alisema Zakaria Hanspope
Aidha Zakaria Hanspope akielezea
kuhusiana na mchezaji Felix Sunzu alisema kuwa masuala ya malipo ndiyo yameleta
utata kati yao
“Felix Sunzu anataka tumlipe pesa kubwa
zaidi ambayo ni dola 3500, ukingalia bajeti yetu kwa sasa hicho kiwango cha
pesa ni kikubwa na itakuwa kazi kumlipa , kwahiyo tumeakuwa tukibishana katika
malipo, yeye amesimamia kiwango hicho na sisi hatuna uwezo wa kumlipa hicho
kiwango kwa sasa”. Alisema mwenyekiti wa Simba kamatii ya usajili, Zakaria
Hanspope
No comments:
Post a Comment