Huu ndio muonekano mpya wa bandari ya Zanzibar, eneo la bandari ya
malindi hasa lile eneo la boti ndogo ziendazo kwa kasi.
Kutokana na
Serikali kutokuwa na uwezo hali iliyopelekea kushindwa kuliendeleza
iliamua kumkabidhi mfanya biashara mzalendo, Bw Said Bakhresa.
Eneo hilo wakati lilipokuwa chini ya serikali lilikuwa kama gofu tu maana halikuwa na hadhi hata ya kuitwa bandari, lakini baada ya kumkabidhi Said Bakhresa mabadiliko yalianza kuonekana kwa muda mfupi na sasa jengo limependeza na naweza thubutu sema hakuna jengo la bandari linalofanana na hilo Tanzania.
Serikali iliweza kufanya jambo la maana kwa kumkabidhi Bwana Said Bakhresa kulifanyia marekebisho hilo jengo, na pia hata kwa maeneo mengine ambayo serikali inaona haiwezi kuyakarabati, basi ikabidhi wazalendo wa hapa nchini wanaoweza kuyarekebisha.
No comments:
Post a Comment