Watu kumi na tatu wanashikiliwa na Jeshi la
Polisi Mkoani Dodoma kwa tuhuma za
mauaji yanayohusisha imani za kishirikina.
Watu hao wanashikiliwa kutokana na tukio la
mauaji lililotokea siku ya Jumatano tarehe 09/01/2013 majira ya saa 04:00
mchana katika kitongoji cha Mtakuja kata ya Chitemo katika Wilaya ya Mpwapwa.
Katika tukio hilo walisababisha kifo cha mtu mmoja aliyefahamika
kwa jina la NELSON S/O NYAGULU mwenye umri wa miaka 32, mkulima wa Chitemo kwa kupigwa na risasi ya Bunduki aina ya
Gobore tumboni na mtu aliyefahamika kwa jina la RASHID S/O KALANI.
Uchunguzi wa awali
unaonyesha kwamba tarehe 08/01/2013 huko katika kijiji cha Chitemo kulikuwa na
mnada, ambapo mvua ilinyesha sehemu moja ya kitongoji cha Mtakuja, sehemu
ambayo alikuwa anaishi mzee mmoja
aliyejulikana kwa jina la LEONARD S/O NYAGALU, Miaka 70, Mgogo.
Kwa vile mvua hiyo
haikunyesha sehemu kubwa katika kitongoji hicho inasemekana Mwenyekiti wa
Kijiji JAVAN S/O MZAZI, Miaka 40, Mgogo, aliibua hoja kuwa kwa nini mvua
inyeshe eneo moja tu analokaa Mzee huyo na kuacha kunyesha sehemu nyingine katika
eneo hilo na kuwahamasisha wenzake kwenda kwa Mzee Nyagalu akawaeleze vizuri.
Majira ya 23.00 hrs
usiku wakakusanyana na kuelekea kwa Mzee
Nyagalu, Walipofika Mzee huyo alisikia watu wakizungumza nyumbani kwake
hivyo akavunja ukuta na akatoroka.
Inadaiwa kuwa kundi
hilo lililokuwa limeongozana na Mwenyekiti wa Kijiji hicho waliingia ndani ya
nyumba na kumkuta mke wa Mzee Leonard Nyagalu na kuanza kumpiga ili aonyeshe
aliko mume wake, waliposhindwa kumpata wakabomoa nyumba na kuichoma moto.
Wakati wanafanya
tukio hilo, walijitokeza watoto wa Mzee Leonard S/O Nyagalo, mmoja wao akiwa ni
NELSON S/O NYAGALU, Miaka 32, Mgogo na ndipo nao wakaanza kupigwa.
Kwa mujibu wa watu
walikuwa katika tukio hilo walisema ilisikika sauti ya mtu mmoja aliyefahamika
kwa jina la RASHID S/O KARANI akisema sasa mmetangaza vita na akafyatua gobore
na risasi zikampata NELSON S/O NYAGALU tumboni zilizopelekea kupoteza maisha
wakati anapata matibabu.
Baada ya kufyatua
risasi toka katika gobole Bw. RASHID S/O KARANI aliwaaga wenzake kuwa anakwenda
kujisalimisha Polisi lakini hadi sasa hajaonekana na jitihada za kumtafuta
pamoja na silaha aliyotumia zinaendelea.
Majina ya
wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi kutokana na kushiriki katika tukio hilo ni kama ifuatavyo:-
1. Dickson S/O Chimosa,
Miaka 52, Mgogo, Mkulima na Mkazi wa Chitemo.
2. Javan S/O Mzazi,
Miaka 44, Mgogo, Mwenyekiti wa Chitemo.
3. Robert S/O Lusije,
Miaka 51, Mgogo, Mkulima na mkazi wa Chitemo.
4. Donald S/O Mponi,
Miaka 33, Mgogo, Mkulima na mkazi wa Chitemo.
5. Daniel S/O Mwamba,
Miaka 24, Mgogo, Mkulima, Mkazi wa Chitemo.
6. Maneno S/O Ngaile,
Miaka 36, Mgogo, Mkulima, Mkazi wa Chitemo.
7. Thomaso S/O Nyagalo,
Miaka 28, Mkulima, Mkazi wa Chitemo.
8. Gilbert S/O Lugaje,
Miaka 39, Mgogo, Mkulima, Mkazi wa Chitemo.
9. Aden S/O Simon,
Miaka 33, Mgogo, Mkulima, Mkazi wa Chitemo.
10.
Malolo S/O Sanja, Mgogo, Mkulima, Mkazi wa Chitemo.
11.
Sospeter S/O Sanja, Miaka 35, Mgogo, Mkulima, Mkazi wa
Chitemo.
12.
Jocktan S/O Chilomo, Miaka 40, Mgogo, Mkulima, Mkazi wa
Chitemo.
13.
Keneth S/O Ngaile, Miaka 38, Mnyamwezi, Mkulima, Mkazi
wa Chitemo.
Aidha
siku ya Jumamosi
tarehe 05/01/2013 majira ya 08:00 asubuhi kulikuwa na tukio la mauji lililotokea katika Kitongoji cha Magungu,
Kijiji cha Mpendo, Kata ya Mpendo Tarafa ya Kwa Mtoro Wilaya ya Chemba Mkoa wa
Dodoma.
Ambapo mtoto mmoja aliyetambulika kwa jina
la TONY S/O SOKOINE mwenye umri wa miaka miwili na nusu (2.5), mkazi wa Kijiji
cha Mpendo alifariki dunia baada ya kujeruhiwa kwa kuchomwa na kisu shingoni
kilichorushwa na mtoto mwenzake aliyefahamika kwa jina la SOMEI S/O REMENDA
mwenye umri wa miaka mine (4) mkazi wa Kijiji cha Mpendo.
Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo
cha Kifo hicho ni kwamba marehemu na mtuhumiwa walikuwa wanacheza nje nyumbani
kwao kwa akina SOKOINE S/O RENENDA ambapo mtuhumiwa alirusha kisu kwa lengo la
kumuua ndege aliyekuwa juu ya mti uliokuwa karibu na nyumba yao, ndipo kisu
huchi kiligonga kwenye mti huo na wakati kinadondoka kilimjeruhi marehemu kwa
kumchoma shingoni na kusababisha kifo
chake.
DAVID A. MISIME - ACP
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA DODOMA |
No comments:
Post a Comment