Mchekeshaji na mwanamuziki wa Bongo Fleva Mussa Yusuf maarufu Kitale amewatolea uvivu wasanii wenzake wa Bongo movie na Bongo Fleva kwa kusema kuwa ni wanafiki na hawana urafiki wa kweli kutokana na tabia waliyoionyesha wakati wa msiba na arobaini ya msanii mwenzao marehemu Hussein Ramadhan Mkieti maarufu Sharo Milionea.
Akiongea kwenye kipindi cha Hotmix cha EATV jana Kitale alisema kuwa aliamua kukaa kimya kwa muda wote tangu ulipotokea msiba ili kupisha shughuli ya arobaini lakini sasa baada ya arobaini hiyo kupita siku ya jumamosi ameamua kutoa ya rohoni.
Kitale amefunguka kuwa hitilafu kwa wasanii hao walianza kuionyesha siku ya msiba walipofika kijijini kwa akina Sharo ambapo wasanii wengi baada ya kufika katika eneo hilo na kuonekana waliwasha magari yao na kuamua kwenda kulala hotelini mjini na kurudi kesho yake siku ya mazishi hali ambayo anasema yeye kwa upande wake hakuifurahia na iliacha maswali kwa baadhi ya watu waliohudhuria kwenye msiba huo.
Kitale ameongeza kuwa katika hali isiyo ya kawaida hali hiyo ya unafiki imejitokeza tena katika shughuli ya arobaini ambapo ilichangiwa na watu watano tu na kuhudhuriwa watu wachche tofauti na ilivyotegemewa ambapo amemtaja na kumpongeza mmoja kati ya wasanii ambae alishiriki kwenye msiba wa Sharo kuanzia mwanzo hadi mwisho kwenye shughuli ya arobaini na kuongeza kuwa ametunga wimbo maalum kwa ajili ya kuzungumzia kifo cha Sharo na kutoa lake la rohoni kwa wasanii wa Bongo movie na Bongo Fleva. | |
|
No comments:
Post a Comment