Thursday, January 10, 2013

AMINI USIAMINI SIJUI KUANDIKA SCRIPT ASEMA JB



Gwiji la filamu za kibongo nchini Jacob Stephen ‘JB’ a.k.a Bonge la bwana, amefunguka kuwa pamoja na ukali wake
katika Tasnia hiyo lakini hawezi na hajawahi kuandika script.

JB ameendelea kufunguka kuwa hana nia mbaya kwa maamuzi yake hayo ila yeye kipaji chake ni kuigiza na mambo mengine katika tasnia hiyo, hivyo hataki kujishughulisha na masuala ya script kwa sababu anatoa nafasi ya ajira kwa wengine kwa kuwa akiamua kufanya kila kitu atakuwa anawakosesha wengine soko na kushindwa kufanya yao.


Kwa mujibu wa JB kazi nzuri ni ile inayopitia kwenye mikono  na watu tofauti wenye ujuzi
na si kila kazi lazima afanye yeye
.

No comments:

Post a Comment