Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Redio Kwizera wilayani Kakonko, Issa Ngumba (45) aliyeuawa enzi za uhai wake. MWANDISHI wa Habari wa Kituo cha Redio Kwizera wilayani Kakonko, Mkoa wa Kigoma, Issa Ngumba (45), ameuawa kwa kupigwa risasi na kunyongwa na watu wasiofahamika.
Habari
zilizopatikana jana zimeeleza kuwa mwili wa mwandishi huyo ulikutwa
porini, siku tatu tangu alipotoweka nyumbani kwake katika mazingira ya
kutatanisha.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Frasser Kashai alithibitisha tukio hilo,
lakini akasema asingeweza kulizungumzia kwa undani kwa kuwa polisi
walikuwa bado eneo la tukio.
Baadhi
ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema mwandishi huyo alikutwa jana akiwa
amekufa, huku mwili wake ukiwa na majeraha ya risasi na ukiwa umenyongwa
na pembeni yake kulikuwa bastola iliyokuwa imetelekezwa pamoja na simu
zake mbili za mkononi.
“Mwili
wake ulipatikana jana katika Pori la Mlima Kajuluheta ulioko katika
Kijiji cha Muhange, Kakonko asubuhi baada ya wananchi kufanya msako wa
siku tatu tangu Jumapili iliyopita ikiwa ni siku moja baada ya kupotea
katika mazingira ya kutatanisha,” alisema mmoja wa mashuhuda hao.
Imeelezwa
kuwa pamoja na vifaa hivyo, pia katika eneo hilo la tukio kulikutwa
risasi tano na katika mfuko mmoja wa suruali ya marehemu, kulikuwa na
noti moja ya Sh10,000.
Mwenyekiti
wa Klabu ya Waandishi wa Habari Kigoma (KPC) Deogratius Nsokolo
alisema: “Sisi ndiyo kwanza tunaelekea eneo la tukio, lakini waandishi
wa Wilaya ya Kibondo ambao waliwahi kufika eneo la tukio na kushuhudia
uchunguzi wa daktari, wameeleza kuwa marehemu amekufa kwa kunyongwa na
kupigwa risasi mkono wa kushoto.”
“Tunaelekea
Wilaya ya Kakonko kutoka Kigoma Mjini, lakini daktari amesema maiti
inaonekana kunyongwa shingo na kupigwa risasi mkononi.”
Alisema mwili huo ulifanyiwa uchunguzi na daktari Primus Ijumaa wa Hospitali ya Wilaya ya Kibondo.
Kamanda
Kashai alisema jeshi lake linasubiri taarifa ya daktari aliyefanya
uchunguzi wa mwili wa marehemu pamoja na taarifa za awali za uchunguzi
kabla ya kutoa taarifa kamili kwa waandishi wa habari.
Naibu
Mhariri wa Kituo cha Redio Kwizera kinachorusha matangazo yake kutoka
wilayani Ngara mkoani Kagera, Seifu Upupu alisema mwandishi huyo
alipotea tangu Januari 5, mwaka huu saa kumi na moja jioni.
“Simu
zake zilikuwa zikiita bila kupokelewa kwa muda wote na hadi jana (juzi)
zikawa hazipatikani kabisa,’ alisema Upupu na kuongeza:
SOURCE:http://uniqueentertz.blogspot.com/ |
Wednesday, January 9, 2013
MWANDISHI WA HABARI AUAWA KIKATILI MKOANI KIGOMA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment