Monday, January 14, 2013

KALA JEREMIAH AIPAKUA ALBUM YAKE YA PASAK

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Kala Jeremiah amezindua rasmi albamu yake ya “Pasaka” usiku wa jana Jijini Dar es Salaam kwa mafanikio makubwa ndani ya ukumbi maarufu wa starehe (Maisha Club), tukio ambalo lilipambwa na michano mbali mbali ya hatari akisindikizwa na Rapa Stamina, Nash MC na Ben Pol.

Kala Jeremiah ambaye alipanda jukwaani kwa muonekano tofauti, aliwanyanyua mashabiki zaidi pale alipopanda jukwaani na bibie Jokate kuimba wimbo wake wa “Ningekuwa rais”, na baada ya hapo akazidi kuwaacha hoi mashabiki baada ya kupiga ngoma yake kali ya “Dear God” ambayo inapendwa zaidi na watu wengi.

Kila la keri Kala Jeremiah na mafanikio mema ya Album hiyo.







No comments:

Post a Comment