Monday, January 14, 2013

OSTAZ JUMA AFUNGUKA KUHUSU BIFU LAKE NA KASSIM MGANGA

Msanii wa Bongoflava, Kassim Mganga ametajwa kumtolea lugha chafu Don anayesimamia kundi la muziki la Mtanashati Entertainment, Ostaz Juma Namusoma (Pichani juu) kutokana na kuchukizwa na kitendo cha Ostaz kumuweka Z -Anto katika wimbo ambayo yeye ameimba kiitikio chake(Chorus) bila ya Kassim kufahamu.

Kwa Mujibu wa Ostaz, Sakata hili lilianza siku si nyingi ambapo Kassim(pichani chini) alidaiwa kumfuata Ostaz na kumuomba kuingia chini ya usimamizi wake, na mchakato wa kufanya kazi pamoja ulipoanza ambapo Ostaz alikubaliana na Kassim kwenda studio kuingiza Chorus na baadae kukubaliana kuwa Ostaz atafute msanii yeyote kwa ajili ya kuingiza Verse ambapo Ostaz aliwatafuta baadhi ya wasanii walioondoka Tip Top Connection akiwemo Z-Anto kwa ajili ya kuingiza Verse na hatimaye ngoma kutoka.
Akizungumza na Blog hii Ostaz amesema baada ya ngoma hiyo kutoka na Kassim kusikia sauti ya Z-Anto kwenye ngoma hiyo ndipo alichukia na kumtolea Lugha chafu Ostaz hata hivyo Ostaz amefunguka kuwa, hakuona sababu ya Kassim kuchukizwa na kutoa Lugha chafu kwa sababu ya kitendo hicho kwa kuwa wakati wa makubaliano yao hakumpa masharti ya aina ya msanii ambae anapaswa kuingiza Chorus na badala yake walikubaliana kuwa atafute msanii yeyote wa kuingiza Verse, Kassim alipotafutwa hakuwa tayari kuzungumza chochote na badala yake alikata simu.

No comments:

Post a Comment