Friday, March 30, 2012

MABALOZI WA NCHI TISA WATEMBELEA MKOA WA MTWARA

MABALOZI tisa wa Umoja wa Ulaya pamoja na mwenzao kutoka Norway walitembelea mkoa wa Mtwara ambapo walifanya mazungumzo na wadau wa maendeleo kuhusu mambo mbali mbali yahusuyo mkoa huo pamoja na shughuli na matarajio ya baadae katika sekta ya gesi asilia.

Ziara hiyo iliongozwa na Balozi Filiberto Ceriani Sebregondi, ambaye ni mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Ulaya kwa Tanzania, ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa kundi hilo. Ilijumuisha wanadiplomasia kutoka katika balozi zilizopo Tanzania za nchi za Ubelgiji, Denmark, Finland, Ufaransa, Ujerumani, Hispania, Sweden na Uingereza. Balozi wa Norway pia alishiriki pia katika ziara hiyo.

Wakuu hao wa balozi za nchi zao hapa Tanzania walitembelea Bandari ya Mtwara, Kisima cha kuchunguza uwepo wa mafuta baharini, mtambo wa kutengeneza gesi na mtambo wa kuzalisha nishati kwa kutumia gesi uliopo jirani na bandari hiyo. Pia walifanya mikutano na maofisa wa serikali mkoani humo akiwemo Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bi. Hasna Mwilima, na wadau wengine.

Tuesday, March 27, 2012

MBUNGE WA JIMBO LA MTWARA MJINI MHESHIMIWA HASNEIN MURJI AWAPIGA TAFU WANAMICHEZO WA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA -MTWARA

Mbunge wa Jimbo la Mtwara mjini (CCM) Mheshimiwa Hasnein Murji amekabidhi vifaa vya michezo na pesa Taslimu Tshs Milioni moja kwa Timu za michezo mbalimbali za Chuo cha Utumishi wa umma mkoani Mtwara kwa lengo la kuzisaidia timu hizo ziweze kufanya vizuri katika mashindano
ya  michezo ya  Vyuo vya Utumishi wa Umma nchini yanayotarajia
kufanyika mwanzoni mwa wiki ijayo Mkoani Tanga ambapo pia ameahidi kutoa kiasi cha Shilingi milioni moja kwa kila mchezo utakaopata ushindi katika mashindano hayo (Pichani :Vifaa vya michezo vilivyotolewa na Mh. Murji)

Mrs Moza Nassor,  Naibu waziri-Serikali ya chuo,Nahodha timu ya Netball

Kufuatia msaada huo,Rais wa Serikali ya wanachuo wa Utumishi
Mtwara,DAISY JAFARI(pichani)  pamoja na NAHODHA  wa Timu ya Netball ambae pia ni
Naibu waziri wa Michezo Chuoni,Bi Moza Nassor kwa pamoja wakiongea na
mdau wa blog hii Abdulaziz Ahmed waliwahakikishia wanachuo pamoja na Wana Mtwara kuwa
timu zao zitarudi na Ushindi kutokana na Ushirikiano walioupata katika
maandalizi ya michezo hiyo itakayoanza April 3 na kumalizika April 6 mwaka huu huko jijini Tanga na kushirikisha wanamichezo 50 kutoka kila tawi la Chuo cha Utumishi wa umma nchini kwa michezo ya mpira wa miguu, mpira wa pete, Volleyball na mpira wa kikapu
Mh. Murji (kulia) akikabidhi pesa taslimu Tshs milion moja kwa Kaimu
mkuu wa chuo, Bw SEME PETER
Mh. Murji akitoa nasaha zake kwa wanachuo
Mh. Murji akionyesha baadhi ya vifaa vya michezo alivyokuja navyo
Mh. Murji akionyesha pesa alizotoa katika kusaidia Timu hizo
Pesa zikikabidhiwa kwa wanachuo wenyewe

MAZISHI YA ALIYEKUWA MKUU WA WILAYA YA LIWALE PAUL CHIWILE

Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, Waziri mkuu Mh.Mizengo Pind, Mkuu wa Mkoa wa pwani Mwantumu Mahiza na Mkuu wa Mkoa wa Lindi wakiwa kwenye mazishi ya aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Liwale Marehemu Paul Chiwile huko Kibaha picha ya ndege
Rais Jakaya Kikwete akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Liwale marehemu Paul Chiwile

Rais Jakaya Kikwete akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Liwale Marehemu Paul Chiwile wakati wa mazishi.

Marehemu Paul Chiwile (kulia) enzi za uhai wake akiwa na mkuu wa wilaya ya Kilwa Nurdin Babu katika moja ya mikutano.

Marehemu Paul Chiwile (kulia) wakati wa uhai wake akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi bw. Ludovick mwananzira wilayani kwake Liwale.
Marehemu Paul Chiwile alifariki ghafla siku ya Ijumaa akiwa katika chumba alichofikia Hotel ya Vision iliyopo Lindi mjini na kuzikwa jana huko nyumbani kwake wilayani Kibaha mkoani Pwani.. Mwenyezimungu ailaze Roho ya marehemu mahali pema peponi, Amina.

Habari: na mdau AbdulAziz Ahmed kutoka Lindi.

ANNA PETER WA EAST AFRICA RADIO ATEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA CHA GUARDIAN ANGEL


Jumamosi iliyopita mtangazaji wa kipindi cha Power Jams ya East Africa Radio, Anna Peter alitembelea kituo cha kulelea watoto yatima cha Guardian Angel kwa ajili ya kufanya mahojiano na Watoto wa kituo hicho pamoja na Uongozi ili waweze kupata msaada wanaouhitaji (Pichani ni Anna Peter akifanya mahojiano na watoto hao)
Anna Peter katika picha ya pamoja na mkurugenzi wa kituo Miriam Msangi(Kulia) pamoja na watoto wanaolelewa katika kituo hicho
Anna, mlezi wa watoto hao pamoja na watoto wenyewe... Watoto hawa bado wanahitaji msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo magodoro, vitanda na chakula hivyo kama unahitaji kutoa msaada waweza kuwasiliana na wahusika kwa namba hizi 0757 855858 na 0655 855858.

MAMBO YA KALUNDE BAND

Weekend niliwatembelea Kalunde Band pale Trititi Hotel Oysterbay ambapo wanapiga kila Ijumaa nikasema nikuonjeshe na wewe yale niliyoyaona mimi walau kwa picha tu
Hicho kinaitwa Kipaji toka moyoni
Raha ya kuimba uimbe kwa hisia kama hivi

Unaambiwa siyo kuimba tu hata kucheza pia wanaweza
Huyu ni mmoja kati ya wanenguaji wao wawili ila huwa wanasafiri sana kwa ajili ya show zingine za Uarabuni, hivyo wanatafuta wanenguaji wengine wasichana wawili wa Permanent ambao watakuwa wanapamba show zao hata kama hao wengine wakiwa wamesafiri Show zao ziweze kunoga si unajua tena wanenguaji nao wana raha yake stejini.. Hivyo kama una mtu unayemjua mkali kwa unenguaji mpe Tip hiyo alambe ajira wanasema undugu ni kufaana na siyo kufanana, mimi nimeplay party yangu na wewe cheza ya kwako kwa kuwaambia wengine usiwe mchoyo.
Hiki ndo kilimuumiza vidole Nape wakati akijifunza kupiga na anasema katika vitu hawezi kuvisahau ni Gitaa, kaka zangu na nyie vipi hakijawaumiza vidole kweli??? hahahhahha
Kipaji hicho kaka, kupiga kinanda na kuimba si mchezo ingawa wapo wengi wanaoweza lakini wapo pia wanaoshindwa.. Salute kwako
Muimbaji na Meneja wa Bendi Deborah Nyange mwenye chuichui, huyu dada ana sauti kama Chirikuu utasikia mambo yake kwenye Afrobeat Kopi kale... Stay tuned
Shabiki mzuka ukampanda nae akaenda kutoa Support kwa mnenguaji.. Usikose mambo haya ndani ya Afrobeat wee endelea kuangalia tu kila Jumamosi saa moja jioni, Jumapili saa 11 jioni na ukikosa kote huko tega jicho lako Jumatano saa 6 mchana.

BONANZA LA WANAHABARI LILIVYOKONGA NYOYO ZETU

Warembo wa FM Academia wazee wa Ngwasum wakipagawisha

2getha 2nawakilisha(Kutoka kushoto ni mimi, Bhoke, Happy na nyuma mwenye pink ni Prudence na Amallu kwa mbaalii) tukiwakilisha EATV Team.

Khadija Kalili kulia wa bongoweekend.blogspot.com na mdau Esther

Wazee wa Ngwasuma wakiendelea kutuonyesha wao ni nani hapa mjini

Mzuka ukiendelea mamaa Happy nae akiwajibika na vimwana wa Ngwasuma

Ikafika zamu ya mgeni rasmi Mh. Sitta kutoa neno lake kwa wanahabari
Burudani ikaendelea yaani ilikuwa hakuna kukaa ni burudani kwa kwenda mbele naona mzee wa kajunason nae akitupa kampan warembo
Kutoka kulia ni Halima, Zamzam, Wilbroad, Sophia na Irene(Wote kutoka Eatv)
Sauda Mwilima kushoto na Irene Moshi wakishow love
Marygoreth Richard na Fadhil Kiwia kutoka dawati la habari
Mkuu wa vipindi Eatv Lydia Igarabuza akishow na Ian Diallo kutoka Breakfast show ya Earadio
Kwa kweli moto uliwaka siku hiyo maana hadi wazee wa Ngwasuma wakapata hofu na kazi yao wakihisi kunyang'anywa
Hapo ni samaki ana vipande vingapiiiii vitatuuuuu, ulikuwa mpambano mkali sana, nikiwakilisha Afrobeat mwenye top nyeupe katikati hapo
Mimi, Prudence Gerald wa 5connect na mamaa Dotnata ambae kampuni yake ilihusika katika suala la msosi
Fatma Nyangasa wa ITV, Halima, Lydia, Irene kwa mbaaali ni Marco Killo na Fadhil
Kutoka Ze Comedy show ya Eatv, kushoto ni Master face, Massawe mtata, Mtanga,Kiwewe na Shabaniii

Hapa ni ile style ya ingia kati tuone kiuno chako na zamu yangu ikafika
Ngwasuma wakapumzika na kuwapisha wanaume TMK nao wakatuonyesha kwa nini wanaitwa wanaume Famili, wakiongozwa na Bibi Cheka
Meza kuu wakifurahia burudani


Msosi timeeeeeeeee
 

Friday, March 23, 2012

AFANDE SELE AWAFUNGUKIA VINEGA

Pichani i Afande Sele(katikati), akiwa na watangazaji wa Super Mix, Zembwela (kulia) na Michael Baruti (kushoto)

Mkali wa Rymes msanii wa Bongo Fleva Dume la Simba Afande Sele amefunguka mengi kuhusu muziki kwa ujumla baada ya kimya cha muda mrefu wakati akizungumza na kipindi cha Super Mix cha East Africa Radio leo, pamoja na shutuma mbalimbali alizopata kuwa yeye ni msaliti wa kundi la Vinega na kudai kuwa yeye na Mh. Joseph Mbilinyi ''Sugu'' ndio waanzalishi wa kundi hilo lakini ''Mchwa'' ants wa kundi hilo ndio wanafiki kwa kuwa wamefanya mengi ikiwemo kumnyima shoo zilizokuwa zikiandaliwa na kundi hilo katika mikoa mbalimbali kama Mbeya na lile la Uzinduzi wa Albam ya Anti Virus lililofanyika katika viwanja vya Ustawi wa jamii hivi Karibuni.


Amemshushia shutuma Soggy Doggy na kusema anamshangaa jinsi alivyo ni mtu wa ajabu na anahitaji kuombewa kwani ni mnafiki na yeye ndio chanzo cha yote haeleweki''.

Afande amesema yeye ni mfalme na kamwe hawezi kuishiwa pamoja na maneno ya shutuma nyingi juu yake za kufeli na kupotea katika Game na hata kuwa anambania Dogo Ditto wakati ni mdogo wake na sasa anafurahia mafanikio na matunda ya Ditto.


Afande Sele pia amefunguka kuhusu muziki wa Bongo Fleva ambapo amesema muziki huo ambao ni shamba sasa limeisha rutuba kwani yamebaki makapi mwanamuziki wa mwisho kuzalishwa kwenye shamba hilo ni Fid Q wanaofuata hawajui nini wanafanya na kuwaita ''Maua Saa sita''


Sele amesema ''Mwanamuziki ni sawa na ua ndani ya bustani kubwa ya Muziki, kazi kwako kuchagua unataka uwe ua la aina gani!! MauaSaaSita Mjipange'' 

DADA AZIMIA BAADA YA KUTAPELIWA SHILINGI 75,000

Dada mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana alipoteza fahamu baada ya kugundua kuwa ametapeliwa pesa kiasi cha shilingi elfu 75 pamoja na simu yake ya mkononi na watu wasiojulikana(Pichani ni akina mama wakisaidia kumnyanyua dada huyo ili kumuweka sehemu salama)

Tukio hilo lilitokea maeneo ya Quality Centre ambapo dada huyo alikwenda kwa matembezi yake ndipo akakutana na vijana wawili ambao walijitambulisha kwake kuwa wanauza madini, dada wa watu akatamani wakaanza kubargain wakafikia bei waliyokubaliana dada akatoa pesa kiasi cha Tshs 75,000 na simu yake ya mkononi ambayo hakusema ni ya thamani gani.
Baada ya wale jamaa kuondoka ndipo akagundua kuwa hayakuwa madini bali ni mawe madogo madogo manne(Pichani ni moja kati ya hayo mawe akiwaonyesha watu waliokuwa kwenye tukio)
Haya nayo ni kati ya hayo mawe manne
Baada ya kugundua kuwa ametapeliwa ndipo akapoteza fahamu, akifikiria simu yake na pesa zake zimepotea bure(Pichani ni huyo dada akisimulia tukio zima lilivyokuwa mpaka yeye kupoteza fahamu)
Baada ya kusimulia mkasa mzima na kupata nguvu dada wa watu huyooo akaondoka.. Huu wizi upo siku nyingi sana na sidhani kama kuna mtu afahamu kuhusiana na hili, sijui tatizo ni tamaa au wengine wageni mjini mimi na wewe hatujui ila la msingi tunatakiwa kuwa makini sana na hili jiji maana kila mmoja ana namna yake ya kutafuta riziki ndo maana wanasema mjini shule........ Ahsanteni wadau Andrew na Angel wa FNB Quality Center kwa picha na habari hii