Friday, November 4, 2011

UNAMKUMBUKA MIRIAM MAKEBA? NI KITU GANI UNAKUMBUKA KUHUSU YEYE? HII NI HISTORIA YAKE FUPI KUHUSU YALE ALIYOYAPITIA KATIKA MAISHA YAKE

Miriam Makeba enzi za usichana wake (huo wimbo "pata pata" ndo uliompatia umaarufu ulimwenguni)

Hapa wakati akiwa na kundi la The skylarks baada ya kuachana na kundi la Manhattan Brothers
Hapo akikamua Stejini



Miriam Makeba ambae pia anafahamika kama mama Afrika” alizaliwa Machi 4, 1932 jijini Johannesburg Afrika kusini na kufariki Novemba 10, 2008. Aliwahi kushinda tuzo ya Grammy kama mwimbaji na mwanaharakati wa haki za kiraia.

Alianza kazi ya muziki kitaaluma mwaka 1950 akiwa na kundi la “south african jazz group”(the manhattan brothers) baadae aliachana na kundi hilo na kuanza kufanya kazi na kundi lake la Skylarks lililokuwa likifanya muziki wa jazz na muziki wa asili ya afrika kusini ambalo lilikuwa la wanawake tupu.

Mwaka 1960 alikuwa msanii wa kwanza Barani afrika ambae aliufanya muziki wa afrika ujulikane huko Marekani na Ulimwenguni kwa ujumla na wimbo ambao ulimpa umaarufu zaidi ni wimbo “Pata pata” ambao aliurekodi kwa mara ya kwanza mwaka 1957 na kuuachia wimbo huo huko Marekani mwaka 1967, (yaani miaka kumi baadae) ambapo alirekodi na kufanya ziara na wasanii wengi maarufu akiwemo Harry belafonte, Paul simon na aliyekuwa mume wake wakati huo Hugh masekela.

Miriam makeba alikuwa akipinga mfumo wa ubaguzi wa rangi Afrika kusini na kuamua kuanzisha kampeni ya kupinga suala hilo la ubaguzi wa rangi katika nchi mbalimbali, jambo ambalo liliikera serikali ya nchi hiyo na kuamua kumfungia uraia wake na haki ya kurudi tena nchini mwake (Afrika kusini) ambapo alirejea nyumbani baada ya ubaguzi wa rangi kumalizika.

Mama wa Miriam makeba alikuwa ni mganga wa jadi na wakati miriam akiwa na umri wa siku 18 mama yake huyo alikamatwa na polisi kwa kosa la kuuza pombe aina ya umqomboti na kuhukumiwa kifungo cha miezi sita jela, hivyo kusababisha maisha ya miezi sita tangu kuzaliwa kwake kuyatumia akiwa gerezani

Mpaka umauti unamkuta Miriam makeba tayari alikuwa na Album 23 ambazo ni pamoja na Patapata, The magic of makeba, The many voices of miriam makeba, Sangoma na zingine nyingi...
Alifariki dunia usiku wa Novemba 10 mwaka 2008 baada ya kufanya onesho katika Tamasha lililoandaliwa kwa ajili ya kumuunga mkono mwandishi Roberto Saviano kutokana na msimamo wake dhidi ya Camorra. 

Hayo ni machache tu kuhusiana na yeye lakini ana historia kubwa sana ya muziki na maisha yake kwa ujumla.

Mwenyezi mungu ailaze roho yake mahali pema peponi... Amina



No comments:

Post a Comment