Tuesday, November 15, 2011

PICHA HIZI NILIZIPIGA WAKATI NILIPOKUWA KWENYE MAFUNZO YA UPIGAJI PICHA MKOANI LINDI








Jamaa akitengeneza mambo yetu yaleeeeee
Hapa akipata kitu baada ya kazi nzito ya kukata miti
Hapa magogo yamekusanywa kwa ajili ya kuchomwa mkaa
Hapo akifanya shughuli ya ukusanyaji magogo
Hili eneo lilikuwa na miti mingi lakini ndo hivyo yote imekatwa
Mwaka jana mwezi wa nne nilikuwa kwenye mafunzo ya upigaji wa picha ambayo yaliandaliwa na FLAME TREE MEDIA TRUST(FTMT) kwa ufadhili wa Tanzania Media Fund(TMF), ambapo waandishi wa habari 15 kutoka mkoani Lindi tulipatiwa mafunzo hayo, na kila mshiriki alitakiwa kuangazia tatizo moja na kulifuatilia kwa upigaji wa picha.

Kwa upande wangu niliangazia suala la uharibifu wa mazingira kwa upande wa ukataji wa miti ovyo na nikachagua kijiji kimoja kinaitwa Likwaya ambacho ni umaarufu kwa uchomaji mkaa huko mkoani Lindi, nilipofika nikatafuta mwenyeji ambae ndo huyo unayemuona kwenye picha juu yeye shughuli yake kubwa ni hiyo ya uchomaji mkaa na familia inapata mahitaji yake muhimu kwa shughuli yake hiyo hiyo.

Nilizungumza nae vitu vingi sana hususani kuhusu suala la uharibifu wa mazingira, hasa nilitaka kufahamu kama ana uelewa wowote kuhusu suala hilo, akaniambia anafahamu vizuri sana madhara ya uharibifu wa mazingira lakini atafanya nini na wakati hana kazi na hiyo ndo shughuli inayomfanya aweze kuishi na kuendesha familia yake?

Mwanzoni aliniogopa kutokana na maswali yangu na zile picha nilizokuwa napiga lakini baadae akawa rafiki yangu tukaanza kupiga story za kawaida tu hadi akaniambia anatumia sigara kubwa na akaitoa na kuanza kuvuta, ikabidi nimuulize kwa nini anatumia hiyo sigara akanijibu kwa urahisi kabisa kuwa inamfanya aondoe uchovu na mawazo maana ile kazi anayofanya ni nzito na anatumia nguvu nyingi sana hivyo inamlazimu kutumia hiyo kitu.
Kazi yangu ilikamilika nikapata kila nilichohitaji na safari ya kurudi mafunzoni ikaanza!! nimeiweka hii habari leo katika kukumbuka tu yale mafunzo na kuwashukuru FTMT pamoja na wafadhili wetu TMF kwa sababu yale mafunzo yamenisaidia kwa kiasi kikubwa sana, lakini pia nina lengo la kushare na wewe kuhusu maisha ya watanzania wenzetu walioko huko vijijini 
lakini kubwa ni jinsi misitu yetu inavyoteketea.

No comments:

Post a Comment