Monday, November 14, 2011

SIRI YA ALLAN MULUMBA MIAKA KUMI NA TANO NDANI YA DIAMOND MUSICA

Rais wa Diamond Musica "Allan Mulumba Kashama"

Kama haumfahamu kwa sura basi hata jina lake utakuwa umeshawahi kulisikia, Allan Mulumba Kashama ni Rais wa sasa wa Diamond Musica Band, ambaye amedumu na Bendi hiyo kwa muda wa miaka kumi na tano sasa tangu enzi hizo ikijulikana kama Diamond Sound Band mpaka sasa.

Nilijaribu kumdodosa ili kujua ni kitu gani kimemfanya aweze kudumu kwa muda mrefu katika bendi hiyo??? akanipa jibu rahisi kabisa kuwa hiyo ni falsafa yake kwa sababu haoni sababu ya kuhangaika katika kila bendi wakati anaona mifano ya wanamuziki wengine wanaofanya hivyo ambapo mwisho wake wanazunguka na kuishia kurudi palepale walipotoka.

Nilipomuuliza ana nini cha kuwaambia wanamuziki wengine wenye tabia hiyo akajibu hana cha kuwaambia kwa kuwa kila mmoja anaishi vile anavyoona kuwa inafaa hivyo na yeye anawaambia waendelee kuishi hivyohivyo kwa kuwa ndivyo wapendavyoo.

Angalia AFROBEAT Jumamosi hii ili uweze kufahamu mengi zaidi kutoka kwake... USIKOSEEEE!!!

Picha kwa hisani ya Global publishers.

No comments:

Post a Comment