Thursday, November 24, 2011

SAUTI YA RADI, MPENZI WA SOKA ASIYESHABIKIA TIMU YOYOTE

Rapa maarufu wa Mashujaa musica Band Yanick Noah a.k.a Sauti ya Radi, ni mpenzi mkubwa sana wa Soka lakini hapendi hata kidogo kuingia uwanjani au kukaa kwenye Runinga na kuangalia mchezo huo.

Akizungumza na Afrobeat Sauti ya Radi amesema yeye ni shabiki mkubwa sana wa mchezo huo wa kandanda lakini anapendelea zaidi kucheza na siyo kutazama kwa kuwa hapendi kuona timu yake ikifungwa, hali ambayo imemsababishia kutokuwa shabiki kabisa wa kuangalia mchezo huo na kutoshabikia Timu yoyote mpaka hivi sasa.

Akizungumzia kuhusu muda wake wa mapumziko amesema muda wake mwingi sana anautumia kwa kutembelea maeneo ya Beach kwa kuwa huko kuna mambo mengi sana ya kufanya kama vile kuogelea na hata kupunga upepo na kuondoa msongo wa mawazo.

Sauti ya Radi ambae ni baba wa mtoto mmoja anajipanga ili aweze kuachana na Bendi na  kufanya kazi zake binafsi kama Solo artist.. Kwa mengi zaidi fuatilia Afrobeat Jumamosi hii.

No comments:

Post a Comment