Thursday, November 24, 2011

LILYAN INTERNET ATOA SOMO KWA WANENGUAJI WENZAKE

Lilyan Internet
Mnenguaji mahiri wa Bendi ya African stars "Twanga pepeta" Lilian Tungaraza maarufu kama Lilyan Internet, amewataka wanenguaji wenzake kuvaa mavazi ya heshima pale wanapokuwa katika matemezi yao ya kawaida ili kulinda heshima ya kazi yao.

Akizungumza na kipindi cha Afrobeat kinachorushwa na Eatv Ting'a namba moja kwa vijana, Lilyan ambae amefunga ndoa mapema mwezi huu amesema watu wengi katika jamii wanaamini kuwa kazi hiyo si ya heshima na wanenguaji wote si watu wanaojiheshimu, hivyo ili kufuta dhana hiyo wanenguaji wenyewe wanapaswa kuonyesha tabia njema hususan kwa upande wa mavazi ili kuifanya jamii iheshimu kazi hiyo na kuichukulia kama kazi zingine.

Ameongeza kuwa wanenguaji wengi wanapenda kuvaa mavazi ya kuonyesha miili yao hata wanapokuwa nje ya kazi na hali hiyo inachangia kwa kiasi kikubwa sana kushusha heshima yao na kuonekana ni wahuni.

Mwisho amewataka watanzania kuichukulia kazi ya unenguaji kama kazi zingine na wazazi wawaruhusu watoto wao kufanya kazi hiyo kwani uhuni ni tabia ya mtu na haihusiani na kazi yoyote.

Kufahamu mengi zaidi angalia Afrobeat jumamosi hii, saa moja kamili jioni.

No comments:

Post a Comment