Thursday, November 3, 2011

CHARLES BABA AFUNGUKA KUHUSU SKENDO ZINAZOMUANDAMA

Charles baba akiwa kikazi zaidi

Katika pozi

Katika pozi na mrembo hapo
Nyota wa muziki wa Dansi nchini anayetumikia Bendi ya African Stars(Twanga pepeta) Charles baba amefunguka na kuzungumzia maisha yake upande wa shilingi ukiachana na kazi yake ya muziki.

Akizungumza na kipindi cha AFROBEAT kinachorushwa na EATV kila jumamosi saa moja jioni, Charles baba alisema yeye hajihusishi na shughuli nyingine yoyote tofauti na muziki kwa sababu kwa sasa anaamini kazi yake hiyo inamtosheleza katika kukidhi mahitaji yake na ya familia yake kwa ujumla.

Muda wake wa mapumziko anautumia kwa kutunga nyimbo kwa ajili ya Bendi yake ya Twanga pepeta na nyimbo zake binafsi kama Solo Artist, na katika kupumzisha akili baada ya kazi za mchana kutwa muda wake wa jioni anapendelea kutembelea katika viwanja mbalimbali vya hapa jijini si unajua tena hapa jijini kuna viwanja viiiiingiiii vya kukufanya ujiliwaze.

Jamani na yeye pia ni shabiki wa michezo mbalimbali lakini hupendelea zaidi Soka (Mpira wa miguu) na kwa hapa nyumbani yeye ni mnazi wa Timu watoto wa Jangwani (Yanga) lakini kwa kule majuu hushabikia zaidi Mashetani wekundu wa Sir Alex Ferguson Manchester United(MAN U).

Pamoja na hayo yooote lakini kubwa ni hili hapa, ana watoto wawili ambao kila mmoja amezaliwa na mama yake ambao wote hayuko nao kwa sasa ila ana mchumba mwingine ambaye anaitwa Salma mtoto wa kiarabu, na kama mungu akipenda anatarajia kufunga nae ndoa mara tu ujenzi wa nyumba yake utakapokamilika, hivyo kama ulikuwa unamnyemelea basi ndo imeshakula kwako jamaa kawahiwa.

Nikamuuliza kuhusu Skendo zinazonakshi magazeti yetu pendwa mara kwa mara zina ukweli wowote??? akanijibu eti ni za uzushi hazina ukweli wowote ila jamaa tu wanatengeneza storiii!!! haya kaka yangu Richard manyota, Issa Mnally, Mateja na wengineo mmesikia maneno ya Charles baba??? je yana ukweli wowote??? haya ukweli wa hili jambo mwaujua nyieeeeee.......

Hayo ndiyo machache kuhusu Charles baba Kingunge ila kwa mengi zaidi tegesha jicho lako Jumamosi hii saa moja jioni katika Ting'a lako namba moja kabisa kwa vijana EATV pekeeeeeee....

No comments:

Post a Comment