Saturday, November 26, 2011

TUNGO ZA MIAKA HII ZINAHARIBU MUZIKI WA TAARAB: SABAH SALUM MUCHACHO

Muimbaji gwiji wa muziki wa Taarab Sabah Salum Muchacho wa Zanzibar Stars Modern Taarab amewaonya waimbaji wenzake kuzingatia Tungo wanazotungiwa kabla ya kuziimba.

Akizungumza na Afrobeat muimbaji huyo mwenye sauti ya kusisimua amesema Muziki wa Taarab tangu zamani ulikuwa na mashabiki wengi na uliheshimika sana kutokana na waimbaji wake kuwa makini na kuzingatia kile walichokiimba tofauti na sasaambapo watunzi na waimbaji wengi wamekuwa hawako makini na Tungo zao

Amesema kipindi cha nyuma Tungo za taarab zilikuwa na mafumbo hata kama unamsema mtu hakuweza kugundua kama yeye ndo anasemwa lakini sasa hivi Mtu anasemwa na anafahamu kuwa yeye ndo mhusika wa wimbo huo naye atajibu kwa mtindo huohuo jambo ambalo linaharibu muziki huo kwa mashabiki wanaouelewa muziki huo.

Aidha amewataka watunzi na waimbaji wenzake kuzipitia Tungo zao kabla ya kuingia Studio na Kurekodi ili kuepuka Tungo zenye ujumbe ulio wazi kwa mashabiki wao kwani kwa kufanya hivyo wanasababisha kuushusha na kupunguza ladha ya muziki huo, hata hivyo amesema kwa upande wake anaona muziki wa Taarab umepoteza muelekeo wa waanzilishi ambapo sasa imekuwa ni mipasho na siyo Taarab kama ilivyokuwa zamani..

1 comment:

  1. mm nampnda xn sabah kuanzia yy mwnyw mpk nyimbo zke na km kna uwezekano wwt wa kueza kucontact nae bc naomba kuijua njia ya kuwacliana nae

    ReplyDelete