Monday, November 28, 2011

SIKU YA TELEVISHENI DUNIANI

Novemba 21 kila mwaka ni siku ya Televisheni Duniani hivyo sisi EATV tuliandaa kipindi maalum kwa ajili ya kuadhimisha siku hiyo ambapo tulitoa nafasi kwa watazamaji wetu kushiriki pamoja nasi kwa kutoa maoni yao kuhusiana na siku hiyo na wangependa nini kifanyike katika kuboresha Televisheni duniani!

Hosts wa show hiyo maalum tulikuwa mimi (Kijah) kushoto na Deo kulia

Tulikuwa na wageni pia studio ambao tulishiriki nao kwenye kipindi ambapo pamoja na mdahalo ambao tulikuwa tukiujadili siku hiyo unaosema ni yupi Presenter bora kati ya mwanaume na mwanamke, pia tulirusha makala kutoka kwa baadhi ya wadau wetu wa Televisheni ambao ni TCRA, Kampuni ya simu za mkononi TIGO, MCT, Chuo cha watayarishaji wa vipindi IAMCO na Makala kutoka BBC ambazo zilieleza mambo tofauti tofauti kuhusiana na Televisheni.

Mmoja kati ya mafundi mitambo wa EATV Allan Lyimo akihakikisha mambo yanakwenda sawa

Timu nzima ya watayarishaji wa vipindi nao wakihakikisha kila kitu kinakwenda sawa

Baadhi ya wageni wetu wa siku hiyo, kutoka kushoto ni Joyce Kiria, Leyla Ledd ambae alimuigiza Salama J anavyotangaza na alipatia saaana, anayefuata ni Lucy kutoka ubalozi wa Uholanzi, Deo na Kijah

Baada ya kipindi kumalizika Team nzima tukapiga picha za ukumbusho maana show ilikuwa tight sanaaaaa

Mauzo yakiendelea



Nikianza kutaja majina hapa tutakesha jamani mniwie radhi
Nikiwa na mmoja kati ya wageni wetu Mr. Reinfared Masako mtangazaji mkongwe wa TV Tanzania ana miaka 30 sasa katika hii Tasnia, nikajisogeza na mimi si wanasema fuata nyuki ule asali labda na mimi nitafika alipo.. inawezekana bhana ila jitihada za makusudi zinahitajika
Mamaa wa wanawake Live nae akasema mmh na mimi nijisogeze japo kwa picha tuuu
Joyce na Deo wakafunga kazi na hadithi ikaishia hapooo

Saturday, November 26, 2011

TUNGO ZA MIAKA HII ZINAHARIBU MUZIKI WA TAARAB: SABAH SALUM MUCHACHO

Muimbaji gwiji wa muziki wa Taarab Sabah Salum Muchacho wa Zanzibar Stars Modern Taarab amewaonya waimbaji wenzake kuzingatia Tungo wanazotungiwa kabla ya kuziimba.

Akizungumza na Afrobeat muimbaji huyo mwenye sauti ya kusisimua amesema Muziki wa Taarab tangu zamani ulikuwa na mashabiki wengi na uliheshimika sana kutokana na waimbaji wake kuwa makini na kuzingatia kile walichokiimba tofauti na sasaambapo watunzi na waimbaji wengi wamekuwa hawako makini na Tungo zao

Amesema kipindi cha nyuma Tungo za taarab zilikuwa na mafumbo hata kama unamsema mtu hakuweza kugundua kama yeye ndo anasemwa lakini sasa hivi Mtu anasemwa na anafahamu kuwa yeye ndo mhusika wa wimbo huo naye atajibu kwa mtindo huohuo jambo ambalo linaharibu muziki huo kwa mashabiki wanaouelewa muziki huo.

Aidha amewataka watunzi na waimbaji wenzake kuzipitia Tungo zao kabla ya kuingia Studio na Kurekodi ili kuepuka Tungo zenye ujumbe ulio wazi kwa mashabiki wao kwani kwa kufanya hivyo wanasababisha kuushusha na kupunguza ladha ya muziki huo, hata hivyo amesema kwa upande wake anaona muziki wa Taarab umepoteza muelekeo wa waanzilishi ambapo sasa imekuwa ni mipasho na siyo Taarab kama ilivyokuwa zamani..

Thursday, November 24, 2011

SAUTI YA RADI, MPENZI WA SOKA ASIYESHABIKIA TIMU YOYOTE

Rapa maarufu wa Mashujaa musica Band Yanick Noah a.k.a Sauti ya Radi, ni mpenzi mkubwa sana wa Soka lakini hapendi hata kidogo kuingia uwanjani au kukaa kwenye Runinga na kuangalia mchezo huo.

Akizungumza na Afrobeat Sauti ya Radi amesema yeye ni shabiki mkubwa sana wa mchezo huo wa kandanda lakini anapendelea zaidi kucheza na siyo kutazama kwa kuwa hapendi kuona timu yake ikifungwa, hali ambayo imemsababishia kutokuwa shabiki kabisa wa kuangalia mchezo huo na kutoshabikia Timu yoyote mpaka hivi sasa.

Akizungumzia kuhusu muda wake wa mapumziko amesema muda wake mwingi sana anautumia kwa kutembelea maeneo ya Beach kwa kuwa huko kuna mambo mengi sana ya kufanya kama vile kuogelea na hata kupunga upepo na kuondoa msongo wa mawazo.

Sauti ya Radi ambae ni baba wa mtoto mmoja anajipanga ili aweze kuachana na Bendi na  kufanya kazi zake binafsi kama Solo artist.. Kwa mengi zaidi fuatilia Afrobeat Jumamosi hii.

LILYAN INTERNET ATOA SOMO KWA WANENGUAJI WENZAKE

Lilyan Internet
Mnenguaji mahiri wa Bendi ya African stars "Twanga pepeta" Lilian Tungaraza maarufu kama Lilyan Internet, amewataka wanenguaji wenzake kuvaa mavazi ya heshima pale wanapokuwa katika matemezi yao ya kawaida ili kulinda heshima ya kazi yao.

Akizungumza na kipindi cha Afrobeat kinachorushwa na Eatv Ting'a namba moja kwa vijana, Lilyan ambae amefunga ndoa mapema mwezi huu amesema watu wengi katika jamii wanaamini kuwa kazi hiyo si ya heshima na wanenguaji wote si watu wanaojiheshimu, hivyo ili kufuta dhana hiyo wanenguaji wenyewe wanapaswa kuonyesha tabia njema hususan kwa upande wa mavazi ili kuifanya jamii iheshimu kazi hiyo na kuichukulia kama kazi zingine.

Ameongeza kuwa wanenguaji wengi wanapenda kuvaa mavazi ya kuonyesha miili yao hata wanapokuwa nje ya kazi na hali hiyo inachangia kwa kiasi kikubwa sana kushusha heshima yao na kuonekana ni wahuni.

Mwisho amewataka watanzania kuichukulia kazi ya unenguaji kama kazi zingine na wazazi wawaruhusu watoto wao kufanya kazi hiyo kwani uhuni ni tabia ya mtu na haihusiani na kazi yoyote.

Kufahamu mengi zaidi angalia Afrobeat jumamosi hii, saa moja kamili jioni.

Tuesday, November 22, 2011

DECEMBER TIPS!!!!! BE CAREFUL...

DEC 22- Payday
DEC 23
DEC 24
DEC 25
DEC 27
JAN 02
JAN 03
2 all Employees, Watch out






Monday, November 21, 2011

USIKOSE KUANGALIA WANAWAKE LIVE SEASON 2 LEO SAA 3 KAMILI USIKU

Mwanamke mtoto mwaya (hapo akituonyesha kilichomfanya aende mapumziko, ndo huyo baby Lincoln)
Madam Ritha nae atakuwepo pia kwenye kipindi hiki cha leo ambapo yeye ndo atafungua pazia la Season 2 kwa upande wa waalikwa
Mamaa wa 8020 fashions na Amina Plummer a.k.a Amina Design nao pia utawaona, najua una hamu kubwa ya kufahamu wamezungumzia kitu gani basi tega jicho lako leo saa 21:00 usiku
Kutoka kushoto ni Dk.Marina Njelekela ambae ni mkurugenzi Hospitali ya Taifa Muhimbili, Shamim, Nasra na Amina Design hao wote watakuwepo kwenye kipindi leo
Baada ya kipindi kumalizika wageni wote na mwenyeji wao wakapata picha ya pamoja, amekosekana Madam Ritha tu kwa kuwa aliwahi kuondoka kutokana na majukumu
Kipindi kiko Hot sana ili usipitwe na uweae kufahamu nini ambacho kimezungumzwa basi kaa karibu na TV yako leo saa 21:00 usiku ni EATV Tinga namba moja kwa vijana pekee......




Sunday, November 20, 2011

SHANGWE ZA EPIQ NATION NDANI YA MTWARA

Nyomiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

Wakaweka shida chini na kurusha mikono juuuuuuuuuu

Soldier mwasiti ndani ya nyumba hapo mbele yake ni Kimanyo Camera man wa Eatv

Hakunaga la Sumalee kama kawaaaa ndani ya Mtwara

Roma mcatholic

Dj Mackey mkuu wa kazi akiwajibika

Thursday, November 17, 2011

NA MTWARA PIA WAPOOOOOO

Anaitwa Dogo Das, ni msanii wa kitambo kidogo na ni maarufu mkoani Mtwara lakini hakupata nafasi ya kushine katika sehemu zingine. Ametoka na ngoma yake inaitwa BADO MAPEMA ambayo oimefanyika katika Studio za K.P Production na mzigo umesimamiwa na Producer Jofu Master kutoka pande hizo hizo za Mtwara.
Dogo anahitaji support yetu sisi wadau wa muziki na mwenyewe anategemea kuwa ngoma hii ndo itamtoa baada ya kusota kwa muda mrefu bila ya mafanikio. Support yako wewe mdau ni muhimu sana kwa huyu dogo!!! Hata MTWARA PIA WAPOOOO.....

Wednesday, November 16, 2011

Tuesday, November 15, 2011

PICHA HIZI NILIZIPIGA WAKATI NILIPOKUWA KWENYE MAFUNZO YA UPIGAJI PICHA MKOANI LINDI








Jamaa akitengeneza mambo yetu yaleeeeee
Hapa akipata kitu baada ya kazi nzito ya kukata miti
Hapa magogo yamekusanywa kwa ajili ya kuchomwa mkaa
Hapo akifanya shughuli ya ukusanyaji magogo
Hili eneo lilikuwa na miti mingi lakini ndo hivyo yote imekatwa
Mwaka jana mwezi wa nne nilikuwa kwenye mafunzo ya upigaji wa picha ambayo yaliandaliwa na FLAME TREE MEDIA TRUST(FTMT) kwa ufadhili wa Tanzania Media Fund(TMF), ambapo waandishi wa habari 15 kutoka mkoani Lindi tulipatiwa mafunzo hayo, na kila mshiriki alitakiwa kuangazia tatizo moja na kulifuatilia kwa upigaji wa picha.

Kwa upande wangu niliangazia suala la uharibifu wa mazingira kwa upande wa ukataji wa miti ovyo na nikachagua kijiji kimoja kinaitwa Likwaya ambacho ni umaarufu kwa uchomaji mkaa huko mkoani Lindi, nilipofika nikatafuta mwenyeji ambae ndo huyo unayemuona kwenye picha juu yeye shughuli yake kubwa ni hiyo ya uchomaji mkaa na familia inapata mahitaji yake muhimu kwa shughuli yake hiyo hiyo.

Nilizungumza nae vitu vingi sana hususani kuhusu suala la uharibifu wa mazingira, hasa nilitaka kufahamu kama ana uelewa wowote kuhusu suala hilo, akaniambia anafahamu vizuri sana madhara ya uharibifu wa mazingira lakini atafanya nini na wakati hana kazi na hiyo ndo shughuli inayomfanya aweze kuishi na kuendesha familia yake?

Mwanzoni aliniogopa kutokana na maswali yangu na zile picha nilizokuwa napiga lakini baadae akawa rafiki yangu tukaanza kupiga story za kawaida tu hadi akaniambia anatumia sigara kubwa na akaitoa na kuanza kuvuta, ikabidi nimuulize kwa nini anatumia hiyo sigara akanijibu kwa urahisi kabisa kuwa inamfanya aondoe uchovu na mawazo maana ile kazi anayofanya ni nzito na anatumia nguvu nyingi sana hivyo inamlazimu kutumia hiyo kitu.
Kazi yangu ilikamilika nikapata kila nilichohitaji na safari ya kurudi mafunzoni ikaanza!! nimeiweka hii habari leo katika kukumbuka tu yale mafunzo na kuwashukuru FTMT pamoja na wafadhili wetu TMF kwa sababu yale mafunzo yamenisaidia kwa kiasi kikubwa sana, lakini pia nina lengo la kushare na wewe kuhusu maisha ya watanzania wenzetu walioko huko vijijini 
lakini kubwa ni jinsi misitu yetu inavyoteketea.

WANAWAKE LIVE SEASON 2




Mwanamke kitenge babu hasa wa kiafrika
Kwenye mazoezi pia wanawake tupo mwanamke unapaswa kujiweka fit

Wanawake Live Season 2 inakuja hivi karibuni kaa tayari kuipokea, kama kawaida inaletwa kwenu na Joyce Kiria kupitia Ting'a namba moja kwa vijana (WANAWAKE LIVE, KUMKOMBOA MWANAMKE KIMAPINDUZI)

TWANGA PEPETA KUSHEHEREKEA MIAKA 50 YA UHURU LONDON


Kundi la muziki wa Dansi nchini, African Stars "Twanga pepeta" wanatarajia kupiga show kali jijini London Uingereza katika kusherehekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.
Akizungumza na Blog hii kiongozi wa kundi hilo Luiza Mbutu, amesema baada ya watanzania kuupokea vizuri uzinduzi wa Album yao ya kumi na moja waliyoiita "DUNIA DARAJA" sasa wameamua kupeleka mashambulizi katika jiji la London ili kujumuika na watanzania wanaoishi huko katika kusherehekea miaka 50 ya nchi yao ya Tanzania.

Show hiyo kali itapigwa siku ya Jumamosi ya Novemba 26 mwaka huu ambapo album yao mpya na za zamani pia zitauzwa kwa wapenzi watakaozihitaji.

Monday, November 14, 2011

SIRI YA ALLAN MULUMBA MIAKA KUMI NA TANO NDANI YA DIAMOND MUSICA

Rais wa Diamond Musica "Allan Mulumba Kashama"

Kama haumfahamu kwa sura basi hata jina lake utakuwa umeshawahi kulisikia, Allan Mulumba Kashama ni Rais wa sasa wa Diamond Musica Band, ambaye amedumu na Bendi hiyo kwa muda wa miaka kumi na tano sasa tangu enzi hizo ikijulikana kama Diamond Sound Band mpaka sasa.

Nilijaribu kumdodosa ili kujua ni kitu gani kimemfanya aweze kudumu kwa muda mrefu katika bendi hiyo??? akanipa jibu rahisi kabisa kuwa hiyo ni falsafa yake kwa sababu haoni sababu ya kuhangaika katika kila bendi wakati anaona mifano ya wanamuziki wengine wanaofanya hivyo ambapo mwisho wake wanazunguka na kuishia kurudi palepale walipotoka.

Nilipomuuliza ana nini cha kuwaambia wanamuziki wengine wenye tabia hiyo akajibu hana cha kuwaambia kwa kuwa kila mmoja anaishi vile anavyoona kuwa inafaa hivyo na yeye anawaambia waendelee kuishi hivyohivyo kwa kuwa ndivyo wapendavyoo.

Angalia AFROBEAT Jumamosi hii ili uweze kufahamu mengi zaidi kutoka kwake... USIKOSEEEE!!!

Picha kwa hisani ya Global publishers.