Warembo wanaowania Taji la Miss Tabata katika picha ya pamoja
Shindano la kumsaka mrembo wa Tabata, Miss Tabata 2012, litafanyika Juni 1 mwaka huu katika ukumbi wa Da West Park, Tabata.
Mratibu wa shindano hilo Joseph Kapinga
amesema kuwa katika onyesho hilo pia kutakuwa na sherehe kabambe ya
kusherehekea miaka 10 ya Miss Tabata.
“Shindano la mwaka huu litakuwa ni la
aina yake kwa sasabu hii itakuwa ni mwaka wetu wa 10 kuandaa shindano hili la Miss Tabata hivyo tutakuwa na burudani nyingi kutoka nje na ndani ya nchi. Pia
tutahakikisha tunashirikisha warembo bomba wenye hadhi ya kushinda taji
la Miss World,” Alisema Kapinga mratibu wa Bob Entertainment na
Keen Arts.
Aidha Kapinga alisema kuwa warembo waliowahi
kushinda mataji tofauti tofauti ya shindano hilo pia watakuwepo
kusherekea miaka 10 ya Miss Tabata.
Warembo watakaoshiriki kwenye shindano wanaendelea na mazoezi kila siku katika ukumbi wa Dar West Park.
|
No comments:
Post a Comment