Thursday, May 3, 2012

MFAHAMU TANZANIA ONE(MSICHANA ALIYEONGOZA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2012

Anaitwa Faith Asenga(Ndiye msichana aliyeongoza katika matokeo ya kidato cha sita mwaka huu)
Leo alikuja katika ofisi za Eatv kwa ajili ya mahojiano na kipindi cha  Breakfast cha East Africa Radio, nasi wengine pia tulipata nafasi ya kuzungumza nae, kikubwa zaidi amesema kuwa mpaka hapo alipofika ni jitihada zake mwenyewe ndizo ambazo zimezaa matunda hayo kwa kuwa alikuwa anajua umuhimu wa Elimu hivyo kwa kutambua hilo ilimbidi ajitume sana na kuweka nia ya kufanya vizuri katika masomo yake ili aweze kutimiza ndoto zake za kuwa Civil Engineer kama mungu akimjaalia maana hilo ndilo lengo lake kubwa sana na ndilo lililomsukuma yeye kuchukua mchepuo wa Sayansi, pamoja na mengi aliyozungumza pia amewataka wanafunzi wenzake kuwa na ushirikiano, waheshimu kila mtu wao kwa wao, wazazi wao na waalimu pia maana heshima ndiyo msingi wa kila kitu na mwisho amewataka wajitume na wawe na ndoto za kuwa watu fulani(Pichani juu akizungumza na Allan Lucky wa Skonga)
Faith hakuja peke yake(Pichani juu ni yeye "Faith" na wazazi wake) pia na wao walizungumza ya kwao ambapo wamewataka wazazi wenzao waige mfano wao kwa kuwa karibu na mtoto wao, wawape ushirikiano wa kutosha na kufuatilia maendeleo yao shuleni.Aidha wameongeza kuwa wamepata faraja kubwa kwa matokeo ya mtoto wao kwani wanaamini yeye kama msichana amepitia changamoto nyingi sana lakini ameweza kuzivuka hivyo wasichana wengine waige mfano wake.

No comments:

Post a Comment