Friday, May 11, 2012

KUELEKEA SIKU YA MAMA DUNIANI MAY 13, TUPAMBANE NA UNYANYASAJI WA WANAWAKE

Mapenzi haya ni ya kizamani jamani, mwanamke hapigwi kwa ngumi hupigwa kwa maneno matamu yenye upendo na wengine husema mwanamke hupigwa kwa kitenge cha Wax
Huyu kamwagiwa maji ya moto na mume wake eti kisa kamnyima unyumba, sasa baada ya kummwagia maji na kumjeruhi kiasi hiki ndo alipewa huo unyumba? Jamani wanaume kama mkeo/mpenzi wako hajisikii kufanya tendo hilo na unaona huna jinsi umezidiwa basi mpe maneno matamu mkeo/mpenzio ya kumshawishi na kumlainisha ili akuelewe siyo kumfanyia matendo ya kinyama namna hii.. Huu ni unyanyasaji, wanawake kwa pamoja tushirikiane kuutokomeza unyanyasaji wa namna hii.
Hivi baada ya kitendo kama hiki unawezaje hata kunuangalia usoni tena mkeo? Tujitahidi kuzuia hasira zetu na kama amekushinda basi muachane kwa usalama na siyo kutiana vilema visivyo na sababu..... Picha: kwa hisani ya

No comments:

Post a Comment