Wednesday, May 23, 2012

CHARLES BABA AMSHANGAA SAJENT

Rais wa Bendi ya mashujaa musica yenye makazi yake jijini Dar es salaam, Charles Baba Kingunge (pichani juu), amefunguka kuwa namshangaa sana mzazi mwenzake Husna Idd a.k.a Sajent kwa tabia yake ya kumfuatilia na kutangaza kuwa bado ana uhusiano na mzazi mwenzake huyo wakati walishamwagana miaka miwili iliyopita. Akizungumza kupitia kipindi cha HOTMIX kinachorushwa kupitia EATV Charles alisema kuwa Sajent kwa sasa ana mpenzi wake na yeye(Charles) anaheshimu hilo lakin i anashangaa kuona mwenzake hataki kukubaliana na hilo na kumfanyia fujo kila msichana anyesikia kuwa ana uhusiano nae. Wakati huohuo Charles amekiri kumwagwa na Mlimbwende Wema Isaack Sepetu na kudai kuwa hajui sababu iliyomfanya mrembo huyo ammwage akidai kuwa labda ameona mapungufu kwake.
Husna Idd a.k.a Sajent

No comments:

Post a Comment