Friday, May 11, 2012

LUIZA MBUTU AFUNGUKA KUHUSU KUONDOKA KWA MCD

Baada ya kimya cha muda mrefu, Kiongozi wa Bendi ya African Stars (Twanga pepeta) Luiza Mbutu (Pichani juu) amefunguka kuhusu kuondoka kwa aliyekuwa mpiga tumba wa muda mrefu katika bendi hiyo (MCD) na kujiunga na Bendi ya Mashujaa Musica. Akizungumza na blog hii Luiza amesema kuwa kwa upande wake yeye kama kiongozi wa Bendi na mtu aliyefanya nae kazi kwa muda mrefu amesikitishwa sana na hapendi kuona mtu akiondoka kwenye bendi hiyo lakini hawezi kumzuia mtu kufanya kile anachofikiria ikiwa ni pamoja na kuhama bendi na kuongeza kuwa wakati wowote yeye(MCD) na wanamuziki wengine walioihama Bendi hiyo wakijisikia kurudi wanakaribishwa kama walivyomkaribisha Muumini Mwinjuma, Badi Bakule na wengineo ambao waliondoka na kurudi.



Naye aliyekuwa mwanamuziki wa zamani wa Bendi ya African Revolution(Tamtam) iliyokuwa ndugu na African Stars ambaye sasa amejiunga na Bendi hiyo ya African Stars Badi Bakule(Pichani juu) amesema ameamua kujiunga na Bendi hiyo kwa kuwa anachukulia kama nyumbani kwa kuwa kampuni ya Asset inayomiliki Bendi hiyo ndiyo iliyomtoa na kumpa umaarufu mkubwa kipindi cha nyuma hivyo ameamua kurudi nyumbani baada ya kugundua kuwa kipaji chake kinapotea kwa kuwa Bendi za T.O.T na Laventure Musica alizokuwa akifanya nazo kazi kabla ya kuamua kujiunga na Twanga zilikuwa hazifanyi maonyesho na kufanya mashabiki wake wasimsikie tena..Hata hivyo mahojiano haya utayaona Liiiveee kupitia Kipindi cha Afrobeat, kaa tayari.


No comments:

Post a Comment