Tuesday, May 15, 2012

HOTMIX YA EATV PREMIER

Show mpya ya Eatv (HOTMIX) imeanza jana 14.05.2012 ikiwa na presenters wapya, kama ilivyo kawaida ya EATV yaani hawajawahi kuonekana kwenye TV yoyote hapa Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla, Show hii itakuwa inaruka kila Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia Saa 11 jioni mpaka Saa moja na itakuwa LIVEEEE
Baadhi ya wageni ambao walizindua Show yetu, (kulia ni Amani Mdimu shabiki mkubwa wa Simba SC na kushoto ni Bhoke Egina mwakilishi wa BBA Tanzania-2011)
Paul Sifael (Kushoto), Mhariri wa Ijumaa wikienda nae pia alikuwa ni mmoja kati ya wageni wetu na kushoto ni Kijah Assistant Producer wa HOTMIX
Presenters wa HOTMIX kutoka kushoto ni Fatna Ramole, Adrian Hillary na kulia ni Anna Mbajo
Baada ya show kumalizika ilikuwa ni kujifotoa tu, pichani ni Team nzima ikijifurahia baada ya kazi nzito

No comments:

Post a Comment