Tuesday, July 16, 2013

Prezzo:SIWEZI MUOMBA DIAMOND MSAMAHA

Habari kutoka Kenya ni kwamba msanii Prezzo amesema hatoweza kumuomba msamaha msanii kutoka Tanzania Diamond Platinumz  kwa kuwa yeye Diamond ndiye aliyeanza kumkashifu Prezzo.

Leo mchana Prezzo akiongea na ‘Mzazi’ Willy M. Tuva’s award-winning show, alisema “Mimi sipendi kuwa na adui kwa sababu muziki unafaa kuleta muungano, sa me
nikashangaa mbona huyu brother ananiingilia na huku sikumbuki kumkosea wala hatujawahi kukutana ana kwa ana”.
Prezzo aliendelea kusema “Mtu yeyote anamjua Prezzo ni kama rattle snake, ukimchokoza you have to get prepared to be bitten.


nilijaribu kumpigia simu lakini jamaa hakupokea simu nikaona ah! Basi liwalo na liwe, nikadecide ku-air my views”, revealed Prezzo.
Aliendelea kusema “Mimi siwezi kumuomba msamaha Diamond kwenye twitter na wala sitoweza kufanya hivyo kwa sababu ni utoto”.

No comments:

Post a Comment