Monday, July 15, 2013

CHADEMA kufungiwa usajili isipoifuta 'Red brigade' .

Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa chini ya mwenyekiti wake Bwana John Tendwa imesema imesikitishwa na Chama cha CHADEMA kuanzisha kambi za mafunzo ya ulinzi (Red Brigade).


Ofisi hiyo ya msajili imekitaka chama cha CHADEMA kuachana na mpango wa mafunzo ya vikundi mara moja vinginevyo ofisi hiyo itakichukulia hatua kali, na hatua hiyo ni kukifutia usajili.


Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari imewataka wale wote wanaosema kuwa CCM inavyo vikundi vya ulinzi, wapeleke ushahidi huo na wao kama wasajili wa vyama vya siasa watakifungia bila kusita.


No comments:

Post a Comment