Friday, July 12, 2013

PAULINE ZONGO, JOAN NA KIMOBITEL WAIBUKA NA NDEGE WA3


Hatimaye wanamuziki wakali nchini Tanzania waliotamba sana hapo nyuma kidogo wameunda kundi lao jipya linalojulikana kwa jina Ndege wa3, kundi jipya  linaloundwa na wanamuziki Joan matovolwa, Khadija Mnoga (Kimobitel) na Paulyne Zongo.

 Wanamuziki wakali haoa hivi karibuni wameshatoa kibao chao kinachokwenda kwa jina la 'MISUKOSUKO YA MAPENZI' ambacho redio kadhaa nchini zimeanza kukirusha.

MISUKOSUKO YA MAPENZI wamesema ni nyimbo ambayo imetungwa kwa umahiri wa hali ya juu, na kuonyesha viwango vya juu katika uimbaji na utunzi, na maudhui ya wimbo huu ni kuonyesha jinsi mapenzi yalivyo na majaribu katika maisha ya kila siku na jinsi ya kuikabili.

Kwa sasa Joan Matovolwa na Paulyne Zongo ni wanamuziki huru wakati Khadija Mnoga (Kimobitel) ni mwanamuziki anayeimba katika bendi ya Extra Bongo inayoongozwa na Camarade Ally Choki.

Mbali na wimbo huo, ndege 3 wamesema kuwa wamejipanga sana kwa nyimbo kali kutoka kwao , maana wamesema sauti za kuimba wanazo , uwezo wa kuimba wanao na sababu ya kuimba pia wanayo

No comments:

Post a Comment