Tuesday, July 2, 2013

OBAMA AONDOKA NA USAFI WA DSM

Rais Barack Obama aliondoka Tanzania jana kurejea nchini kwake Marekani na tukihesabu tangu muda aliiondoka hadi sasa ni masaa machache tu yameshakatika, lakini ukiangalia jiji la Dar es Salaam chini ya mkuu wa mkoa wake Bwana Said Meck Sadiki hali ya jiji imeendelea kurudi kama zamani kabla hajaja Bwana Barack Obama.

Naomba niinukuu kauli ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam aliyoitoa wakati jiji la Dar es Salaam linajiandaa na mapokezi ya Obama alisema hivi


'Naomba wananchi waelewe kwamba usafi tunaofanya sasa katika jiji la Dar es Salaam sio sababu ya ujio wa Rais Barack Obama na marais wengine wa nje waliotutembelea kwa sasa, ila hii ni kampeni iliyokuwepo toka zamani kuwa sasa ni wakati wa kusafisha jiji hili, kwahiyo ujio wa wageni hawa umetukuta wakati tunatekeleza kampeni yetu ya kusafisha jiji la Dar es Salaam".


Swali wanalouliza wananchi ni hili. Je, hayo yalikuwa na maneno tu ya kuwadanganya ili wamuamini mkuu huyo wa mkoa kuwa sasa jiji la Dar es Salaam litakuwa safi zaidi ya manispaa ya Moshi inayoaminiwa kwa usafi Tanzania.


Afro Kija leo asubuhi ilizungumza na baadhi ya wakazi na walikuwa na maneno haya ya kuzumngumza.


"Mimi nakaa Kigamboni na ninafanya kazi maeneo ya Palm Beach, zamani kabla ya ujio wa Barack Obama tulikuwa tumezoea kununua maandazi pale Posta kwaajili ya vitafunwa, wakati wa maandalizi ya Obama wale wauzaji wakapigwa marufuku kuuza pale na wakaondoka, lakini leo nashangaa nimepita pale asubuhi nimewakuta na nimenunua maandazi yake kama kawaida. hii inaashiria ule usafi ulifanyika kwaajili ya bwana Obama na sio kuwa walikuwa na mkakati wa usafi jijini" Alisema Musa Kijeba wa Kigamboni Dar es Salaam.


AfroKija haikuishi hapo iliweza kuongea pia na wakazi wa maeneo ya Mwenge na maeneo ya jirani kuhusiana na usafi maana wakati wa ziara ya Obama ni moja ya eneo lililofanyiwa usafi kwa sana.

"Mwenzangu, tena jana nimenunua sketi mbili za mitumba pale jioni maana nilitamani Obama aondoke mapema maana hili ni jiji letu tulishazoea usafi hakuna, kwahiyo hayo masuala ya kusema wana kampeni ya usafi ni uongo, kama kweli haikuwa usafi kwaajili ya Obama kwanini alivyoondoka tu asubuhi jioni yake hawa wauza vigenge na mitumba hapa mwenge wakawa wamerudi?" Aliuliza Jack Massawe mkazi wa Mwenge

Wakazi wengi walitoa maoni yao maana hata wale wauza mitumba wa karume na maeneo mengine wameweza kuerejea katika maeneo yao na kuendelea na shughuli, maeneo ya mwananyamala uchafu nao umeongezeka tena zaidi ya hapo awali. 


Je, Dar es Salaamu usafi bila viongozi wa Marekani haiwezekani??!! Tafakari chukua hatu

No comments:

Post a Comment