Kuhusu baba mzazi wa Joyce Kiria, Michael Francis Lwambo Kiria wa kibosho dakau nganyeni kufariki huko mkoani Tanga ambako alikuwa akiishi, naomba nitoe maneno kidogo ya faraja kwake.
Joyce Kiria Leo ni siku ambayo hutakaa kuisahau maishani mwako, kwa sababu majuzi tu ndo umetoka Tabora kumwona rafikiyo wa karibu sana, mumeo. Leo tena msiba
wa baba yako, Pole sana dada yangu.
Kuna mambo nataka yakufariji; Mungu anaweza kuonekana zaidi wakati wa furaha na amani na wakati wa shida asionekane kabisa.
Hapa nina maana kwamba Mungu yupo pamoja nasi kila wakati ila tunapokuwa na furaha na amani yeye huwa pembeni yetu na ndiyo maana unamuona, lakini tunapokuwa na woga au kupita katika shida na majaribu yeye hutuchukua na kutufunika na uwepo wake na ndiyo maana hatumuoni.So, hupaswi kuogopa chochote kwani yeye atakuvusha kwenye bonde la uvuli (Zaburi 23:1-6).
Joyce, kila jambo linalotokea hapa
duniani liwe zuri au baya, iwe furaha au huzuni fahamu kuwa Mungu karuhusu.
Mungu ndiye ajuaye sababu. Umesikia habari ya Ayubu, ndo maana
tumeagizwa kushukuru kwa kila jambo.
Mwisho, usimtafute mtu yeyote
juu wakati huu ila MUNGU pekee. MUNGU NA AKUSAIDIE.
Mwenyezimungu aiweke roho ya marehemu mzee Michael Lwambo mahali pema peponi, Amina
Mwenyezimungu aiweke roho ya marehemu mzee Michael Lwambo mahali pema peponi, Amina
No comments:
Post a Comment