BAADA ya kuvuliwa urais 'Kocha wa Dunia sasa wanamuziki wawili nguli, Waziri Sinyo na Muumin Mwinjuma, Rais wa zamani wa bendi ya Victoria Sound, wamezichapa kavu kavu live wakati wa mazoezi ya bendi yao yaliyofanyika Mbagala, jijini Dar es Salaam, jana.
Katika kichapo hicho, inadaiwa kuwa Sonyo nusura amchome Muumini kisu, hivyo kuzua hofu katika patashika hilo la aina yake linaloendelea kuonyesha mgogoro mkubwa kati ya wanamuziki hao ndani ya bendi ya Victoria Sound.
Akizungumza muda mchache baada ya sakata hilo, Muumini alisema alishangaa kujikuta yupo chini na Sonyo akiwa ameshatoa kisu kutaka kumjeruhi.
Muda mchache baadaye Muumini aliandika kwenye mtandao wa kijamii akielezea tukio hilo alilodai ni la aina yake huku akitumia lugha kali za kuudhi dhidi ya Sonyo.
“Leo ndio nimedhihirisha huyu (TUSI LIMEHIFADHIWA) ni kweli amenikuta nimekaa tena pembeni na tahadhali zote ila alivyokuja kwangu kunivamia sikumkawiza nikampa ngumi 3 takatifu zilizolenga uso wake ndio akaona kumbe huyu mzima akatoa kisu mfuko wa kulia watu wakamuwahi kumshika, lakini wakati nakwepa kisu nilianguka, na kama sio George Gama angekuwa ameshanijeruhi au kuniua kabisa, ngoja nimfunze adabu nampeleka mahakamani ili iwe fundisho na kwa hili sina msalie mtume hivi jimwili lote la Sonyo Bado anamshikia mwanaume mwenzie Kisu na amshukuru, Janurry aliyenipakata ningempukutisha meno kwa ngumi maana alikuwa kama kuku mgonjwa hakurusha hata ngumi," mwisho wa kunukuu meseji ya Muumini.
Kupigana kwa wanamuziki hao ni mwendelezo wa mgogoro mzito uliokuwapo kwa bendi hiyo baada ya uongozi pia kumuondoa katika nafasi ya urais Muumini na kumpa Kassim Muhumba, huku pia Sonyo akienguliwa katika nafasi yake ya kiongozi wa shoo.
Je ni kweli Kocha wa dunia atajiweka pembeni na kuachana na muziki kama alivyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari hivi karibuni, kama alivyoesema kuwa iwapo Victoria Sound itakufa ama kuondoka katika bendi hiyo, basi ataachana na muziki na matukio haya inawezekana mwanamuziki huyo ameanza kujilaumu kwa kauli hizo TATA.
No comments:
Post a Comment