Thursday, August 15, 2013

Majangili waitisha serikali

SERIKALI imesema mtandao wa majangili wanaoua tembo mkubwa wenye watu walio na uwezo kifedha ambapo wapo ndani na nje ya nchi .

Siri hiyo ilifichuliwa Dar es Salaam jana na Waziri wa Mali Asili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Alisema tayari Serikali ina majina ya mtandao unaojihusisha na biashara ya ujangili wa meno ya tembo na baadhi yao wapo pia wafanyabiashara wakubwa waliopo ndani na nje ya nchi.

"Tayari majina tunayo ya mtandao wa watu wanaojishughulisha na ujangili wa meno ya tembo huu ni mkubwa ambao una pesa nyingi, hauna tofauti na ule wa dawa za kulevya,"alisema

Alisema sio kwamba wameshindwa kufanya kazi bali wanaendelea kupata taarifa na wameandaa operesheni hai itakayosaka wale wote ambao wanahusika na ujangili huo.

Aliongeza kuwa wanaendelea kufuatilia nchi inayonunua meno hayo ambapo nchi zilizopo Bara la Asia ni miongoni mwa zinazo husikana biashara hiyo.Ali sema siorahisi ku shinda vita hiyo kwa kutumia vyombo vya habari.

 "Mnajua hii ni vita kubwa na ni waambie kuwa vita hii huwezi kushinda kwa kutumia vyombo vya habari, hivyo Watanzania kuwe ni na amani na tunajitahidi kuhakikisha tunamaliza tatizo hili,"alisema.

Katika hatua nyingine,alisema mfumo wademokrasia uliopo unachangia kurudisha nyuma jitihada mbalimbali zinazofanywa, kwani watu wakikamatwa na kupelekwa mahakamani kesho yake wanaonekana mtaani.

 Alisema wanaobainika kufanya biashara hiyo ya ujangili hata Polisi wamo na wengine wameshafukuzwa kazi na wengine kusimamishwa, hivyo hizo zote ni jitihada za Wizara yake.Naye Mwenyekiti wa kamati hiyo John Lembei alisema kuwa kamati yake imeiomba Serikali kuondoa kodi ya asilimia tatu ambayo ilipitishwa na bunge kwa ajili ya mfuko wa maendeleo ya utalii na asilimia kumi ambayo yalikuwa yanawasilishwa Serikalini kwani inachangia kuondoa huduma za jamii zilizokuwa zikitolewa kwenye jamii inayozunguka hifadhi hizo.

Alisema kamati imeomba serikali kama kweli wanataka kuendeleza sekta ya utalii basi kodi hiyo ifutwe vinginevyo hifadhi hazitakuwa salama na ujangili utaongezeka kwa kiasi kikubwa.

"Hifadhi hizi za TANAPA na ngorongoro ilikuwa miradi ya kusaidia jamii inayowazunguka kwa kuwajengea shule, hospitali, maji, pamoja na huduma zinginezo hivyo kutokana na bunge kupitisha kodi hiyo wameondoa huduma hizo,"alisema Lembei.

No comments:

Post a Comment