Sunday, August 11, 2013

FEZA kaiaga BBA

Feza Kessy, mtanzania pekee aliyekuwa amebaki katika jumba la Big Brother Africa, amekuwa mshiriki wa 20 kutolewa katika jumba hilo usiku wa leo.

Kwa week 11 zilizopita, Feza aliishi maisha ya kipekee sana ambayo ilikuwa ni aidha unampenda ama unamchukia na si vinginevyo.

Baada tu ya mtangazaji IK kutangaza kuwa Feza ndiye anayeaga mashindano hayo, Feza aliwakumbatia washiriki wengine na kuondoka kuelekea stejini ambako alipofika tu, IK alimtupia swali la kama bado “anampenda Oneal..?” na ndipo Feza akajibu “ndio” bila kusita japo pia alionyesha kuwepo kwa hali fulani ya kutokuaminiana kati yake na Oneal hasa baada ya kukiri kwamba siku za mwanzo Oneal alivutiwa zaidi na mshiriki mwenzie Cleo.

Feza ameondoka na matumaini ya watanzania kuipepea bendera ya ushindi hasa ikizingatiwa kwamba mshiriki mwenzie Nando alitolewa katika mashindano hayo takribani wiki mbili zilizopita kwa kuvunja sheria za Big Brother.

Aliyekuwa sukari wa Feza katika mjengo huo, Oneal, aliyaaga mashindano hayo wiki iliyopita kwa kupata kura chache ukilinganisha na washiriki wenzie waliokuwa kikaangoni ambao ni Feza na Bimp.

No comments:

Post a Comment