Monday, September 2, 2013

Henry Joseph kutambulishwa rasmi

KIUNGO mpya wa klabu ya Simba, Henry Joseph, leo anatarajiwa kuwemo katika kikosi cha timu hiyo kitakachomenyana na Mafunzo ya Zanzibar, katika mechi ya kirafiki kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Joseph amesajiliwa na Simba akitokea klabu ya Kongsvinger ya Norway.

Mechi hiyo itawapa fursa mashabiki wa klabu hiyo kuwaona wachezaji wake wapya wakiwemo, Amisi Tambwe na Gilbert Kaze ambao wote wanatoka katika klabu ya Vital O ya Burundi.


Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga, mechi hiyo ambayo ni ya kwanza kwa Simba kucheza katika uwanja huo itakuwa ni kujiweka sawa kabla ya kucheza na Mtibwa Sugar kwenye uwanja huo, Septemba 14.

Kamwaga alisema mbali ya kutazama mechi hiyo, pia mashabki watapata fursa ya kumuaga mchezaji Kiggi Makasi anayekwenda nchini India kwa ajili ya matibabu ya goti na ataondoka Septemba 9.

No comments:

Post a Comment