Thursday, December 8, 2011

The kilimanjaro Band ilivyoutangaza mlima Kilimanjaro

The kilimanjaro Band
Waziri Ally wa Kilimanjaro Band akifanya vitu vyake

 Naamini ulikuwa hufahamu hata jina la Kilimanjaro Band ( Wananjenje) lilitokana na nini, sasa leo nakufahamisha japo kwa uchache tu kuhusiana na Bendi hiyo.
Kilimanjaro Band hapo mwaka 1973 wakati inaanzishwa iliopewa jina la Revolution Band na ikaendelea kufahamika hivyo mpaka mwaka 1989 Band hiyo ilipopata Safari ya kwenda Uingereza ndipo hapo Idea ya kubadili jina ilipokuja na jina lililofikiriwa ndo lilikuwa hilo The Kilimanjaro Band ikidaiwa kuwa jina la mwanzo la Revolution Band limekaa kizungu zaidi kwa hiyo hata huko waendako wenyeji wangewashangaa ndipo wakaamua kuiita Kilimanjaro wakiwa na maana ya kuutangaza mlima Kilimanjaro.
Na kama mawazo yao yalivyowatuma ndivyo ilivyokuwa maana walipofika huko wenyeji walishangaa sana kusikia Bendi ya Tanzania inatumia jina hilo wakiamini kuwa Mlima huo upo nchini Kenya, hivyo ikabidi wao(Kilimanjaro Band) waanze kuwaelimisha watu kuwa wadhaniavyo siyo sahihi kwani mlima huo upo kwenye ardhi ya Tanzania, ndipo wakaanza kufahamu na ndo hivyo mpaka leo inafahamika hivyo ingawa kuna baadhi ya watu bado wanaamini kuwa mlima huo upo nchini Kenya, hivyo sisi kama Watanzania tunapaswa kutumia nafasi tunazozipata kwa kuutangaza mlima wetu huo na Nchi yetu kwa ujumla..
Maelezo haya ni kwa mujibu wa Wazri Ally mmoja kati wa wanamuziki wa The kilimanjaro Band a.k.a wana njenje ambae aliyaeleza haya yote alipokuwa akizungumza na kipindi cha Afrobeat kinachorushwa na Eatv ambapo tulitaka kufahamu mambo mbalimbali kuhusiana na muziki ndipo pamoja na mengi aliyotueleza tukayapata na hayo kuhusu Bendi yao na akaongezea kuwa jina la Njenje lilitokana na wimbo ule unaoitwa Njenje ambao ulivuma na kupendwa sana na bado unaendelea kupendwa mpaka sasa, hivyo kutokana na mapenzi ya watu kwa wimbo huo ndipo wakaibatiza Bendi hiyo kwa jina la Njenje.




No comments:

Post a Comment