Monday, December 19, 2011

MCT YATOA MAFUNZO KWA WANA EATV


Picha zote hapo juu zinaonyesha wanasemina wakifuatilia mafuzo kwa umakini
Mmoja kati ya wawezeshaji Bi. Haura Shamte mwandishi wa habari wa siku nyingi
Siku ya Jumamosi ya Dec 17, 2011 MCT kwa kushirikiana na EATV waliandaa mafunzo kwa wafanyakazi wa EATV na Radio yaliyolenga kuwakumbusha wafanyakazi wake baadhi ya mambo yanayohusiana na Tasnia nzima ya habari.

Tulijifunza  vitu vingi sana maana wanasema Elimu haina mwisho ingawa kuna watu wana uzoefu mkubwa sana wa hii kazi ya habari lakini nao walipata nafasi ya kukumbushwa baadhi ya vitu muhimu ambavyo havipaswi kusahaulika katika kazi.

Baadhi ya vitu hivyo tulivyojifunza ni pamoja na Namna ya kuandika habari, Ipi stori na ipi siyo stori, maana kuna baadhi ya waandishi wao wanajiandikia tu hata hawaangalii uzito wa hiyo habari,Interview Techniques na hili nalo pia ni muhimu sana maana ukiangalia na kusikiliza vipindi vyetu vingi hapa nchini utaona aibu kutokana maswali yanayoulizwa inaonyesha wazi kuwa watu wamesahau au hawajui namna ya kuuliza maswali.

Pia tulipata bahati ya kufahamu tofauti ya Mwandishi na mtangazaji maana siku hizi mtu akiwa mtangazaji anaitwa mwandishi lakini je hii ni sahihi?? Jibu ni kwamba inategemea maana wanasema mtu yeyote ambaye yuko kwenye Media ni mwandishi sababu wakati mwingine anashiriki kwa njia moja ama nyingine katika upatikanaji wa hiyo habari na wakati huo huo anaweza asiwe mwandishi pia.

Jamani tulijifunza vitu vingi saaaaanaaa nikisema niandike vyote hapa nitawachosha wadau ila Mafunzo haya yataendelea pia Jumamosi ijayo na tutaendelea kufahamishana yale tuliyojifunza.

No comments:

Post a Comment